Header Ads Widget

UTEUZI MPYA: KITILA MKUMBO, PATROBASI KATAMBI WANG'OLEWA, NI BAADA YA KUCHUKUA FOMU ZA UBUNGEProf. Kitila Mkumbo

Leo Julai 17, 2020 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali, wakiwemo wakuu wapya wa wilaya, makatibu wakuu na manaibu katibu wakuu wa wizara mbalimbali.

Miongoni mwa uteuzi huo mpya ni Pamoja na Mhandisi Antony Sanga ambaye sasa anakuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji akichukua nafasi ya Prof. Kitila Mkumbo ambaye amejitosa kwenye hekaheka za kugombea ubunge.

Vilevile, Rais Magufuli amemteua Josephat Paulo Maganga kuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma akichukua nafasi ya Patrobasi Katambi ambaye amechukua fomu ya kuwania ubunge wa Jimbo la Shinyanga kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Pia Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Dkt. Allan Kijazi ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wizara ya Maliasili na Utalii.

Soma zaidi uteuzi huo kwenye taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa, ambapo wateule wote wanatakiwa Ikulu ya Chamwino, Dodoma Julai 20, 2020 saa 4:00 asubuhi kwa ajili ya kuapishwa.