Header Ads Widget

WAGOMBEA UBUNGE NA UDIWANI SHINYANGA WAAHIDI KULETA MABADILIKO MAKUBWA


Mariam Nyanganga ambaye alikuwa Diwani wa viti maalum kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM Kata ya Kitangiri Manispaa ya Shinyanga amejitosa kugombea Udiwani Kata ya Kitangiri,Kata ambayo ilikuwa inashikiliwa na Chadema.
Mwalimu wa chuo Cha St. Joseph tawi la Shinyanga Jimotoli Jilala Maduka akimkabidhi fomu ya kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Agnes Bashemu baada ya kuijaza na kuirejesha.
Enes Zacharia Madata akikabidhi fomu kwa Katibu wa CCM ya  kugombea Ubunge Jimbo la Msalala Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga kuomba ridhaa ya Chama chake kupitishwa kuwa mgombea Ubunge jimbo hilo,ambapo amesema iwapo atapitishwa kuwa mgombea atahakikisha fedha za mfuko wa jimbo kutekeleza miradi ya maendeleo ambayo itaacha alama ya kudumu jimboni kwa kushirikiana na jamii na siyo kuzitumia kusaka kura.
Mariam Nyanganga ambaye alikuwa Diwani wa viti maalum kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM Kata ya Kitangiri Manispaa ya Shinyanga akichukuwa fomu ya kugombea Udiwani Kata ya Kitangiri,Kata ambayo ilikuwa inashikiliwa na Chadema.


Mwalimu Hamisa Boniface wa Manispaa ya Shinyanga akionyesha fomu ya kugombea Ubunge jimbo la Shinyanga 

Mgombea ubunge Jimbo la Shinyanga Frances Gilya  Kasili akirudisha fomu kwa katibu wa chama Cha mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga Agnes Bashemu , mtoto wa mkulima ameamua kugombe ubunge.

Amesema akichaguliwa kuwa mbunge atabadilisha  Shinyanga na kuwa na sura mpya na mfumo mpya wa uwekezaji, kunyanyua hadhi ya wakulima na wafanyabiashara wadogo amesema kwani yeye  kama kijana atafanya mambo makubwa zaidi ambayo kwa sasa ni chamgamoto.
Mgombea ubunge Jimbo la Shinyanga Frances Gilya  Kasili akirudisha fomu ya kugombea Ubunge jimbo la Shinyanga na kumkabidhi katibu wa chama Cha mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga Agnes Bashemu.