Header Ads Widget

LEMBELI: VIJANA HAWANITISHI, NITAPAMBANA NAO

James Lembeli

Na Ali Lityawi -Kahama
JAMES Lembeli ni miongoni mwa wanachama 129 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliochukua fomu katika wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga kuwania ubunge wa Jimbo la Kahama Mjini, ambapo amesema licha ya idadi kubwa ya vijana kujitokeza haogi na yuko tayari kupambana nao.

Lembeli amewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Kahama kwa tiketi CCM (2005 hadi 2015) kisha kuhamia upinzani na kurejea tena chama tawala, ambapo Julai 16, 2020 alijitokeza kuchukua fomu kati ya makada 69 waliochukua fomu hiyo, huku akijimwambafai kupambana na wagombea vijana.

Lembeli aliyechukua fomu hiyo majira ya saa tano za asubuhi katika ofisi ya CCM Wilaya ya Kahama anajaribu kwa awamu nyingine kuwania Ubunge Jimbo la Kahama Mjini.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, mara baada ya kuchukua fomu hiyo, Lembeli alisema kuwa ameamua kugombea Ubunge katika jimbo hilo kwa tiketi ya CCM kwa kuwa vigezo anavyo huku akijinasibu  yupo tayari kupamba na vijana katika uchaguzi huo.

 “Timu ikicheza uwanjani lazima wachezaji wote wawe wazuri na katika mchezo hakuna mzee pia na mimi nipo tayari kwa mapambano ingawa wengi wa wapinzani wangu waliochukua fomu hizo kupituia chama cha Mapunduzi ni vijana,” amesema.

Aidha amesema pindi ikitokea baadhi ya watu kutaka kufahamu alichosahau Bungeni, amedai hakuna alichosahau zaidi ya utashi alionao wa kuhitaji kuwatumikia wananchi wa jimbo la Kahama   pindi akipata ridhaa ya kuwatumikia kwa awamu nyingine.

Kwa mujibu wa Katibu wa CCM wilaya ya Kahama, Emmanuel Mbamange, alisema hadi kufikia jana kuna wana CCM 69 waliochukua fomu katika Jimbo la Kahama Mjini ambapo kati yao Nane ni wanawake.

Mbamange alisema Jimbo la Msalala lina watia nia 43 ambapo kati yao mwanamke ni mmoja,huku Jimbo la Ushetu wakijitokeza 17 miongoni mwao wanawake ni wawili.