Header Ads Widget

WAZIRI NDALICHAKO AZITAKA SHULE BINAFSI KUMALIZANA NA WALIMU WAO WAREJEE KAZINI

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, amewaagiza wamiliki wa shule binafsi kumaliza tofauti zao na walimu ili wanafunzi wa kidato cha sita wapate haki yao ya elimu na kumaliza mitihani yao salama.

Akijibu swali kutoka kwa waandishi wa habari kuhusu baadhi ya shule ambazo walimu wake hawajaripoti licha ya kufunguliwa kwa kidato cha sita, Ndalichako alisema  changamoto za kielimu kati ya mmiliki wa shule na mwalimu zisiathiri taaluma ya wanafunzi.

Ndalichako alisema hayo jana Juni 4, 2020 jijini Dar es Salaam wakati wa kupokea na kukabidhi matanki 100 kutoka Kampuni ya Africab.

Alisema swala la mikataba baina ya mwajiri na mwalimu Serikali haiwezi kuingilia.

“Mikataba baina ya mwajiri na mwalimu, Serikali haiwezi kuingilia, ina wajibu wa kufuatilia vigezo na masharti, ambavyo vimewekwa vinatakiwa kufuatwa ili wanafunzi wapate taaluma stahiki.

“Swala la walimu shule binafsi kutoripoti mashuleni nimechukua na nitalifuatilia, kwa kuwa sijapata taarifa rasmi nitalifuatilia zaidi ila kuna vigezo vya kuwa na shule binafsi.

“Shule inavyosajiliwa inatakiwa kukidhi vigezo na masharti ya Wizara ya Elimu, moja ya sharti ni kuwa na walimu wa kutosha kuwapa taaluma wanafunzi, kwa kuwa wamerejea mashuleni wanatakiwa kupata elimu,” alisema Profesa Ndalichako.


Chanzo: Mtanzania Digital

SOMA ZAIDI>>>

https://mtanzania.co.tz/ndalichako-atuma-salamu-shule-za-kidato-cha-sita-ambazo-walimu-hawajaripoti/



Post a Comment

0 Comments