Header Ads Widget

NAIBU WAZIRI KWANDIKWA AONGOZA HARAMBEE YA KUCHANGIA UJENZI NYUMBA ZA MAPADRI KAHAMA


Na Patrick Mabula - Kahama
Mbunge wa jimbo la Ushetu wilaya ya Kahama ,Elias Kwandikwa ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano mzuri kwa viongozi waliowachagua katika kutatua changamoto mbalimbali za kimaendeleo.

Kwandikwa alitoa wito huo katika harambee ya ukamilishaji wa nyumba ya mapadri wa Parokia ya Watakatifu Petro na Paulo, Nyamilangano Jimbo Katoliki la Kahama mkoani Shinyanga juzi akibainisha kuwa siku zote uongozi ni umoja katika kujiletea maendeleo.

Naye Padri Severine Mshumbusi Paroko wa Parokia hiyo ya watakatifu Petro na Paulo Nyamilango alisema anaipongeza Serikali na kanisa kwa ushirikiano uliopo kwa lengo la kuwatumikia watu na kuwashukuru wale waliojitoa kuchangia ukamilishaji wa nyumba yao, ambapo jumla ys Sh Milioni 13.2 zilipatikana kwenye harambee hiyo

TAZAMA PICHA CHINI
Mkurungenzi wa halmashauri ya Ushetu , Michael Matomola (katikati) akizungumza wakati wa harambee ya kukamilisha nyumba ya mapadri wa Parokia ya Petro na Paulo Nyamilangano jimbo Katoliki la Kahama. kushoto ni Padri Severine Mshumbusi paroko wa parokia hiyo na kulia ni Mwenyekiti wa halmashauri ya Ushetu Juma Kimisha.
Mbunge wa jimbo la Ushetu na Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa akichangisha fedha za kukamilisha nyumba ya mapadri wa parokia ya Milangano jimbo la Katoliki la Kahama.
Padre Severine Mshumbusi paroko wa parokia ya Watakatifu Petro na Paulo Nyamilangano Jimbo Katoliki la Kahama wakati wa harambee ya kuchangia ukamilishaji wa nyumba ya makazi ya mapadri.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Elias Kwandikwa akizungumza na waumini wa Parokia ya Watakatifu Petro na Paulo Nyamilangano jimboni kwake wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa nyumba ya mapadri.

Picha zote na Patrick Mabula - Kahama