Header Ads Widget

RAIS ASEMA HANA MPANGO WA KUANZISHA SINDANO ZA DAWA YA MITISHAMBA


Rais wa Madagascar Andry Rajoelina amebadilisha msimamo wake kuhusu dawa ya nchi yake anayodai kuwa na uwezo wa kutibu corona.

Mwezi uliopita bwana Rajoelina alizindua rasmi dawa ya mitishamba ambayo alisema kwamba ina uwezo kuzuia na kuponya wagonjwa walio na virusi vya corona.

lakini hilo lilipingwa na shirika la afya duniani kwasababu hakuna thibitisho la kisayansi kuhusu dawa hiyo.

Taasisi ya kitaifa ya matibabu nchini Madagascar pia ilitilia shaka uwezo wa dawa hiyo iliotengenezwa kutoka kwa mmea wa pakanga, ikisema huenda ikaathiri afya ya wanadamu.

Lakini licha ya taarifa ya taasisi hiyo , siku ya Jumanne bwana Rajoelina alisema kwamba Madagascar itaanzisha sindano za dawa hiyo huku akiongezea kwamba majaribio yake tayari yameanza kufanywa nchini Marekani.

Hatahivyo Michelle Sahondrarimalala, ambaye ni daktari na mkurugenzi wa tafiti za idara ya mahakama, amefafanua zaidi alichomaanisha rais huyo, akisema kwamba waandishi hawakumuelewa kile ambacho kiongozi huyo wa taifa alitaka kutangaza.

Alisema kwamba hakukuwa na fikra zozote za kuiweka dawa hiyo kutumika kupitia sindano na kwamba kamati ya kisayansi haijafikia uamuzi kama huo.