Mapema Jumatano, melfu ya wanafunzi walirejea shuleni baada ya kufunguliwa
tena nchini humo na kulegeza masharti yaliyowekwa awali kukabiliana na virusi
vya corona
Lakini baada ya siku moja tu, maambukizi mapya 79 yalirekodiwa, ikiwa ni
kiwango cha juu zaidi kwa siku nchini humo kwa kipindi cha miezi 12.
Maambukizi haya mapya yalihusisha watu wa kituo kimoja ambacho kipo nje ya
mji wa Seoul.
Ghala ambalo lililopo mji wa Bucheon, linaloendeshwa na kampuni kubwa ya
kibiashara ya Coupang, na maafisa wanasema sehemu hiyo ilikuwa haitekelezi
kikamilifu hatua za kuzuia maambukizi.
Maafisa wa afya walibaini maambukizi ya virusi vya corona katika viatu na
mavazi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo.
Inawezekana Korea Kusini ikaendelea kurekodi maambukizi mapya wakati huu
inapoendelea kupima maelfu ya wafanyakazi wa kampuni hiyo.
Maambukizi mapya 58 yalirikodiwa siku ya Ijumaa, na kusababisha taifa hilo
kuwa na jumla ya idadi ya watu wenye maambukizi ya corona 11,402.
'Kitovu cha maambukizi'
Jumla ya shule 251 huko Bucheon zimelazimika kufungwa .
Imeripotiwa katika gazeti la Korea Times, kuwa Wizara ya Elimu imesema jumla
ya shule 117 katika mji mkuu wa Seoul pia zimeahirisha tarehe ya kufunguliwa
tena kwa shule.
Mwanafunzi mmoja mjini Seoul ambaye mama yake alikuwa akifanyakazi katika
ghala la kampuni ya Coupang pia naye amepatikana na na virusi vya corona.
Sehemu za umma na maeneo ya historia katika mji wa Seoul zimefungwa,
biashara pia zimefungwa na watu wametakiwa kutafuta namna nyingine ya kufanya
kazi na kuzuia mkusanyiko wa watu wengi.
Korea Kusini ni miongoni mwa mataifa ambayo yalikumbana na athari kubwa ya
mlipuko wa corona mwanzoni mwa mwaka huu lakini ikaonekana kuwa imeweza
kudhibiti janga hilo kupitia mpango wa kutafuta, kupima kutibu watu.
Wiki za hivi karibuni, kumeonekana kuwa na maambukizi mapya kutokea, ikiwemo
tukio moja lililohusisha mwanaume mmoja ambaye alitembelea vilabu vitano vya
usiku mjini Seoul mji wa Itaewon mapema mwezi huu.
Kwa mujibu wa chombo cha habari cha Yonhap, maambukizi mapya 266
yamefuatiliwa kwa karibu huko Itaewon.
Credit-Bbc Swahili
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464