Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga ACP Debora Magiligimba.
Na Suzy Luhende-Shinyanga
Jeshi la
polisi Mkoani Shinyanga kwa kushirikiana na wananchi wa maeneo ya Kijiji cha
Mwakitolyo linamtafuta Mwanamke mmoja ambaye bado hajafahamika jina wala makazi yake kwa kosa la
kumtupa mtoto mchanga.
Kamanda wa Jeshi
la Polisi Mkoani Shinyanga ACP Debora Magiligimba amesema tukio hilo limetokea May 19 Mwaka huu majira ya saa mbili asubuhi huko katika kitongoji cha Mwakitolyo
namba 5 kijiji cha Mwakitolyo tarafa ya Nindo halmashauri ya Shinyanga vijijini
mkoani hapa.
Kamanda Magiligimba amesema kuwa mtoto
asiyejulikana jina jinsia ya kiume na anayekadiliwa kuwa na umri wa siku mbili
tangu kuzaliwa kwake amekutwa akiwa ametupwa na kutelekezwa kichakani na mama
yake mzazi ambaye bado hajafahamika.
Aidha mtoto huyo
mchanga amekutwa akiwa amevilingishwa kwenye Kanga ambapo tayari amepelekwa Zahanati ya Kijiji cha Mwakitolyo na kupewa huduma ya kwanza na hali yake
inaendelea vizuri chini ya uangalizi wa karibu zaidi wa watalaaamu wa huduma ya afya.
Aidha Kamanda wa Polisi Mkoani Shinyanga ametoa rai kwa wakazi wa mkoa huo hususani maeneo ya Wachimbaji wa Madini ya Dhahabu kuendelea kutoa ushirikiano ili kufanikisha kukamatwa kwa Mtuhumiwa huyo ili hatua kali za
kisheria zichukuliwe dhidi yake.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464