-------------
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI)Dkt. Revocatus Mushumbusi amesema wamebaini aina kumi za miti ambayo inauwezo wa kutibu magonjwa mbalimbali ikiwemo kufubaza dalili za awali za ugonjwa wa homa kali ya mapafu COVID 19.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAFORI Dkt. Revocatus Mushumbusi akizungumza na waandishi wa habari katika hifadhi ya misitu Hashi Lubaga Manispaa ya Shinyanga.ambapo amesema kuna miti kumi ya dawa za asili ambayo ni bora zaidi na inatumika sana mikoa ya kanda ya ziwa.
Na mwandishi wetu
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI)Dkt. Revocatus
Mushumbusi amesema wamebaini aina kumi za miti ambayo inauwezo wa kutibu
magonjwa mbalimbali ikiwemo kufubaza dalili za awali za ugonjwa wa homa kali ya
mapafu COVID 19.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa
ziara yake ya kutembelea hifadhi ya
misitu ya asili Hashi eneo la Lubaga Manispaa ya Shinyanga,ambapo shughuli za
utafiti na uoteshaji wa miti zinafanyika amesema miongoni mwa majaribio
yaliyoanzishwa na kusimamiwa kwa uangalifu na taasisi hiyo ni pamoja na jaribio
la mti ya dawa ya asili.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAFORI alisema kupitia utafiti huo waligundua miti ya dawa
ya asili takribani 300 inayotumika
kutibu zaidi ya magonjwa 100 na walipoifanyia uchambuzi miti 10 ilikuwa bora zaidi kutokana na kutumika mara
kwa mara kanda ya ziwa.
“Aina ya
miti hiyo ni Mlungulungu ambayo mizizi
na majani yake yanatibu homa na madonda kwa kujifukiza,Nengonengo inatibu athma(kushindwa
kupumua)ikiwa ni miongoni mwa dalili za Corona,Mzima unatibu homa kali na
Mwatya/mkalya inatibu magonjwa ya ganzi ya mwili,kichwa namatatizo ya tumbo.”amesema
Kaimu Mkurugenzi.
Miti
mingine ni Mlundalunda unatibu matatizo ya tumbo,kifua,ngili,ganzi ya mwili,mti
wa Mfutwambula/ng’wengwambula matatizo ya tumbo,kifua,athma na ngili,mti wa
Msana unatibu mapafu,kikohozi,vidonda vya kooni na miti ya Mondo,Mgada na
Ningiwe yote inatibu matatizo ya presha,tumbo na ganzi.
Kutokana na janga la ugonjwa wa Corona ambalo
mpaka sasa halijapata chanjo wala tiba,mtaalamu wa tiba za asili na muuzaji wa
madawa Mussa Kuhangaika mkazi wa Shinyanga,aliomba wizara ya afya Kuwashirikisha
wataalamu wa tiba mbadala ili kuweza kupata dawa ya aina moja inayotibu Corona.
Naye Kaimu Mkuu wa TAFORI kanda ya ziwa Iddy Dibwa amesema miti ni chanzo kikuu cha dawa za asili
zinazotumiwa na wananchi wengi kutibu magonjwa mbalimbali kanda ya ziwa na
utafiti huo wamefanya ili kutambua dawa za miti shamba zinazotumika sana kanda
hiyo.
Mwisho.