Na Damian Masyenene
JUMLA ya watoa huduma za Afya ngazi ya jamii 109 kutoka Wilaya ya Shinyanga Mkoani humo wamepewa
mafunzo na mbinu mbalimbali za namna ya
kukabiliana na homa kali ya mapafu inayosababishwa na Virusi vya Corona (COVID-19).
Mafunzo hayo yametolewa kwa watoa huduma hao 53 kutoka
halmashauri ya Shinyanga na 56 kutoka Manispaa hiyo yakiratibiwa na Shirika la
Doctors with Africa /CUAMM kwa kushirikiana na Serikali pamoja na idara ya afya
mkoa wa Shinyanga.
Akizindua mafunzo hayo ya Siku tatu kwa watoa huduma za
Afya ngazi ya jamii 53 kutoka halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga yaliyofanyika
leo Mei 23 katika ukumbi wa Liga Hotel iliyopo Mjini Shinyanga, Mganga Mkuu wa Mkoa
huo (RMO), Dk. Yudas Ndungile amewataka wahudumua hao kupeleka taarifa na elimu kwa jamii kwa kutumia mbinu
mbalimbali na siyo kukariri kwenda nyumba kwa nyumba
.
Dk. Ndungile amesema kwamba taifa liko kwenye kipindi cha
kutekeleza na kuendeleza mapambano dhidi ya Corona hivyo wadau wasilale na
kubweteka.
“Tuko
hapa kuelezana wajibu wetu katika mapambano dhidi ya Corona na nini tunatakiwa
kufanya katika maeneo yetu, tuwe wabunifu tunapokuwa tunatekeleza majukumu yetu
kwa mbinu mbalimbali siyo lazima mpite nyumba kwa nyumba tusome kwanza
mazingira ya maeneo yetu na tufanye kazi kwa kushirikiana na maofisa afya,
watendaji wa kata,vijiji na viongozi wa wafanyabiashara katika maeneo ya
minada, masoko, nyumba na vibanda vya kukatisha tiketi,” amesema Dk. Ndungile.
Katika hatua nyingine, Dk. Ndungile amewataka wadau na
wataalam wa afya kuhakikisha kwamba wanaendelea kuwaelimisha na kuwasisitiza
wananchi kuendelea kupata huduma na matibabu katika magonjwa mengine huku
wakiendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Covid
19.
“Mbali na Corona
sisitizeni pia wagonjwa waendelee kwenda hospitali kupata matibabu mfano
wajawazito kwenda kliniki, watoto wapate chanjo, wenye VVU, kifua kikuu na
Malaria kwahiyo wadau warudi kazini wananchi waendelee kukumbushwa na kusisitizwa
namna ya kufuata matibabu kwa tahadhari,” amesema.
Kwa upande wake Mratibu shughuli za kijamii mradi wa
upimaji na matibabu kutoka Shirika la Doctors with Africa/ CUAMM, Gasaya Msira ameeleza
kuwa kutokana na shughuli mbalimbali kuathiriwa na janga la Corona waliona
umuhimu wa kushiriki kuisaidia jamii kupata elimu licha ya wao kujihusisha zaidi
na masuala ya Virusi Vya Ukimwi (VVU).
Msira amesema kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya kwanza ya jitihada zao kwani wamepanga kuyafanya kuwa
endelevu kulingana na miongozo itakayokuwa inatolewa na Wizara ya Afya kuhakikisha
kuwa wanatoa taarifa kila inapohitajika na kuwa na uwezo mkubwa wa kuisaidia
jamii.
“Tunapenda kuona
wahudumu wengi zaidi wanafikiwa na mafunzo haya, tuko tayari kuendelea kupanua
wigo na kuwafikia watoa huduma ngazi ya jamii wengi zaidi kwa sababu mbali na
mafunzo tunawapa barakoa na tunashirikiana na mkoa kutoa vifaa kinga,” amesema
Msira.
Msira ameongeza kuwa wao kama Shirika lisilo la kiserikali
ni wajibu wao kuhakikihsa wanashirikiana na Serikali katika Mapambano mbalimbali ndani ya sekta ya
afya ili jamii iweze kuelimika sambamba na kuchukua tahadhari katika suala zima
la Magonjwa yanayoikumba jamii.
kwa upande wake Meneja Miradi wa Doctors with Africa/CUAMM Francesco Bonanome amesema kuwa shirika hilo litaendelea kushirikiana na serikali katika kuhakikisha kuwa huduma bora za afya zinaendelea kutolewa na serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo walioko mkoani Shinyanga.
kwa upande wake Meneja Miradi wa Doctors with Africa/CUAMM Francesco Bonanome amesema kuwa shirika hilo litaendelea kushirikiana na serikali katika kuhakikisha kuwa huduma bora za afya zinaendelea kutolewa na serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo walioko mkoani Shinyanga.
Nao baadhi ya washiriki ambao wamehudhuria mafunzo hayo, akiwemo
Rafael Kamuli kutoka Kijiji cha Jomu Kata ya Tinde wamesema kuwa watayatumia mafunzo
na elimu waliyoipata kuisaidia jamii inayowazunguka hasa kwa kuzingatia kwamba maeneo yao kuna Shughuli
mbalimbali za Kijamii ikiwemo, Minada,Masoko,biashara mbalimbali hivyo mafunzo hayo ni muafaka kwa kuinusuru
jamii yao.
Mafunzo hayo yameanza kutolewa Jumatano hadi Ijumaa kwa
watoa huduma ngazi ya jamii 56 kutoka Manispaa ya Shinyanga na kuendelea tena leo Mei 23 hadi Mei 25 kwa watoa
huduma 53 kutoka halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ambao baada ya mafunzo hayo watakwenda
kusaidia kutoa elimu na taarifa kwa
jamii.
Bw Gasaya Msira Mratibu wa shughuli za kijamii mradi wa upimaji na matibabu toka Shirika la Doctors with Africa/CUAMM
Hilda Maginga Afisa Jamii Shirika la Doctors with Africa/CUAMM akitoa neno kwa Washiriki wa mafunzo.
Meneja Miradi wa Shirika la Doctors with Africa/CUAMM Bi Veronica Censi anayemaliza muda wake wa utumishi nchini akiwaaga washiriki wa Mafunzo hayo na kuwatakia Maisha mema
Kulia ni Francesco Bonanome Meneja Mpya wa Shirika la Doctors with Africa/CUAMM akifuatilia kwa umakini ushiriki wa Watoa huduma.
Mganga mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dr Yudas Ndungile akiwatakawashiriki kuwa wabunifu katika utoaji wa elimu na taarifa.
Bw Gasaya Msira Mratibu wa shughuli za kijamii mradi wa upimaji na matibabu toka Shirika la Doctors with Africa/CUAMM akitoa neno kwa washiriki wa Mafunzo wahudumu wa afya ngazi ya jamii toka halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Mwita Thomas Mratibu wa elimu ya Magonjwa ya mlipuko Mkoa wa Shinyanga akiendelea kutoa elimu kwa washiriki.

Afisa Afya Mkoa wa Shinyanga Bi Neema Simba akiendelea na utoaji wa elimu ya namna ya kukabiliana na Covid 19 kwa watoa huduma ngazi ya Jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Washiriki wakiendelea na Darasa
Washiriki wakisikiliza ujumbe wa mgeni rasmi
Baadhi ya Washirki wa Mafunzo wakiendelea kufuatilia kwa ukaribu toka kwa watoa elimu.
Mwandishi wa habari wa Shinyanga Press Club Damiani Masyenene akiendelea kumhoji mmoja wa Washiriki na kufahamu namna watakavyokwenda kuisaidia jamii katika kipindi hiki cha Covidi 19.
TAZAMA ZAIDI PICHA MBALIMBALI KATIKA MATUKIO




Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464