Header Ads Widget

MMOJA AFARIKI BAADA YA MOTO KUTEKETEZA KAMBI YA WAVUVI

 Baadhi ya wakazi na wavuvi wa kisiwa cha Muchangani Kata ya Kome halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema wakiangalia jinsi moto uivyoathiri mali zao. 



Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Maria Bundala (40) amefariki dunia huku magari matano na vibanda zaidi ya 150 kuwaka moto baada ya moto kuzuka katika kambi ya wavuvi ya Kisiwa cha Kome kilichopo wilayani Sengerema Halmashauri ya Buchosa.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, ACP Muliro Jumanne Muliro, amesema eneo hilo lina Mkusanyiko wa watu zaidi ya elfu 3,000 huku Shughuli kubwa ikiwa ni uvuvi.  "Majira ya saa 6:1 usiku kulitokea tukio hilo ambapo baada ya kufika eneo hili tumebaini mtu mmoja anayejulikana kwa jina la Maria Bundala (40) amepoteza maisha huku magari zaidi ya manne aina ya fuso na vibanda vilivyojengwa katika mfumo wa kufanya kazi mbalimbali na makazi vikiteketea kwa moto,." amesema Kamanda Murilo
Kamanda Murilo amesema Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama wanafanya tathimini ili kujua ni kwa kiwango gani cha athari kimetokea huku  usalama ukiimarishwa katika eneo hilo.   
Noel Sangija ni mmoja wa wakazi waliokubwa na adha hiyo amesema janga hilo limesababishwa na mamalishe kusahau kuzima moto baada ya kupika chakula kwani moto ulipo anzia ndipo mafiga yalipo , hivyo waliiomba serikali kuwatengenezea mpango mkakati wa unjezi mzuri ili kujinusuru na majanga kama hayo.
“Tumeuguza samaki  zenye gharama kubwa hii ni mara ya tatu majanga kama haya yananikuta ambapo mara ya kwanza aliunguza gesti mbili ,mara ya pili na kipindi hiki ameunguza gesti yenye vumba 24 ,mwanzoni tulikuwa na utaratibu wa kuzunguka kwa wale wanaopika karibu na makazi ya watu”anasema Sangija.  
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mangella, Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Emmanueli Kipole ametembelea eneo hilo akiwa na kamati ya ulinzi na usalama mkoa kwa lengo la kuhakikisha usalama unaimarishwa katika eneo hilo.
Kama ilivyo katika matukio kama haya kuna baadhi ya watu wasio na utu wanaona hii ni fursa kwao hivyo natoa onyo kwa watu mwenye tabia hizo waache na vitu vilivyookolewa vibaki salama sihitaji kuona mtu anafanya mambo ya hovyo  kamati ya usalama mkoa na wilaya itakuwepo hapa hadi mambo yawe shwali” amesema Kapole
Amewataka wakazi wa eneo hilo kurejea katika vijiji vyao ili mahali hapo palekebishwe lakini watambue Serikali inatambua michango yao katika kujenga taifa na itakuwa pamoja nao.
 Chanzo IPP MEDIA/Nipashe.