
Baadhi ya viongozi wa Klabu ya Simba wakizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam

Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba, Senzo Mbatha akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waaandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Na Damian Masyenene na Mitandao
ILE hamu ya mashabiki na wadau
wa soka nchini iliyokuwa inasubira kufahamu nini kitajiri leo saa 7 mchana
kutoka klabu ya Simba, hatimaye
imejibiwa ambapo Wekundu hao wa Msimbazi wametangaza kuanza kujifua rasmi
Jumatano Mei 27, mwaka huu.
Simba SC wametangaza uamuzi huo
kupitia kwa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Senzo Mbatha leo saa 7 mchana katika
mkutano wao na wanahabari jijini Dar es Salaam baada ya kuweka kibwagizo kwa
takribani siku tatu kikiwaacha njia panda mashabiki ambao walisubiria kufahamu
ni nini kitajiri.
"Tumeanza mipango yetu na
tumepanga kuanza mazoezi Jumatano baada ya Eid."- CEO Senzo Mbatha
Mbatha raia wa Afrika Kusini
ameweka wazi kuwa wachezaji wote wa tmu hiyo waliopo nje ya nchi tayari
wamefanya mawasiliano nao na wataanza kuwasili kabla mazoezi hayajaanza siku ya
Jumatano.
"Wachezaji wetu wote ambao
wapo nje ya Tanzania tunawasiliana nao na mmoja kati ya wachezaji hao atakuwepo
nchini Jumatatu. Wengine tunatarajia watakuwepo nchini kabla hatujaanza
mazoezi."- CEO Senzo Mbatha.
"Lazima tujikite
kuhakikisha tunashinda ligi kuu na FA. Hiyo ndio dhamira wetu kwa sasa."-
CEO Senzo Mbatha.
Katika hatua nyingine Klabu
hiyo ya mitaa ya Msimbazi imezindua rasmi tovuti yake ambayo itakuwa na habari,
matukio na Ratiba, timu, historia ya klabu, matukio yote ya klabu, sehemu ya mashabiki,
huku wakiweka wazi kuwa watazindua App ya klabu hiyo wiki ijayo.
Wekundu wa Msimbazi Simba SC
ambao ni mabingwa watetezi wa Lgi Kuu Tanzania bara wanaongoza ligi kwa tofauti
ya pointi 17 wakiwa kileleni na alama 71 wakifuatiwa na Azam FC yenye pointi 54
na Yanga yenye alama 51, ambao kutangaza kuanza mazoezi kwa tmu hiyo ni mwitikio
wa tamko la Serikali kuruhusu michezo kurejea ifikapo Juni Mosi, mwaka huu.