Header Ads Widget

DIWANI AKAMATWA NA TAKUKURU AKIGAWA FEDHA KWA WAJUMBE WA UWT MSIBANI


Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa mkoani Mbeya inamshikilia diwani wa viti maalum katika Halmashauri ya wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya kwa tiketi ya CCM ,Tumaini Mwakatika kwa tuhuma za kutoa rushwa kwa wajumbe wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake UWT wilayani Kyela. 

Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mbeya,Julieth Matechi,wakati akizungumza na waandishi wa habari . 

Amesema diwani huyo alikamatwa Mei 30,mwaka huu akigawa fedha kwa wajumbe hao kwenye msiba wa Mwenyekiti wa UWT,wilayani Rungwe,Ester Mwakipesile ambaye alifariki dunia hivi karibuni. 

Matechi amesema uchunguzi wa awali wa TAKUKURU umebaini kuwa mtuhumiwa alikuwa akigawa fedha kwa wajumbe ambao walikuwa wamefika kuhudhuria ibaada ya mazishi ya marehemu Ester. 
 Aidha,amesema katika mahojiano yake na TAKUKURU ilidhihirisha kuwa kuna viashiria vya rushwa katika tukio hilo na kwamba uchunguzi unaendelea na mtuhumiwa amewekwa rumande kituo cha polisi Kyela.