` FARU KAZINI: RHINO RANGERS YAJIAÑDAA KUMVAA STAND UNITED SHINYANGA

WANDAMAN HOTEL

FARU KAZINI: RHINO RANGERS YAJIAÑDAA KUMVAA STAND UNITED SHINYANGA

 



Tabora

Klabu ya RHINO RANGERS yenye maskani yake mkoani Tabora inaendelea na mazoezi yake kuikabili Stand United, mchezo unaotarajiwa kupigwa jumamosi ya October 03, 2026 majira ya saa 10:00 jioni katika uwanja wa CCM kambarage, Shinyanga.

Makamu mwenyekiti wa Rhino Rangers Bandora Salum Mirambo amewataka mashabiki kuendelea kuipa timu sapoti katika mechi zijazo ili kuongeza hali ya morali na kujiamini kwa wachezaji na benchi la ufundi.

Bandora amesema mashabiki wakiwa mstari wa mbele, timu inapata nguvu ya kupambana na kupata matokeo mazuri.

Kituo kinachofuata ni Shinyanga kwa Rhino Rangers kuwakabili Stand United.


RHINO RANGERS "Safari yetu ya ushindi inaendelea".
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464