` MISA TANZANIA WATEMBELEA MELI KUBWA YA MV NEW MWANZA AMBAYO IMETAJWA KUWA KICHOCHEO KIKUBWA CHA UKUAJI WA UCHUMI WA NCHI

WANDAMAN HOTEL

MISA TANZANIA WATEMBELEA MELI KUBWA YA MV NEW MWANZA AMBAYO IMETAJWA KUWA KICHOCHEO KIKUBWA CHA UKUAJI WA UCHUMI WA NCHI

 



Na Marco Maduhu, MWANZA

Wanachama wa Taasisi ya vyombo vya habari kusini Mwa Afrika Tawi la Tanzania MISA TAN, wametembelea katika Mel ya MV NEW Mwanza, ambayo imetajwa kuwa ni miongoni mwa miradi mikubwa ya kuchochea ukuaji wa uchumi nchini, kutokana na kuunganisha nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kurahisisha usafiri na kukuza mwingiliano wa kibiashara.

Ziara hiyo imefanyika leo Oktoba 13,2026 ikiongozwa na Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Edwin Soko.

Akizungumza wakati wa kutoa taarifa kwenye ziara hiyo
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Kampuni ya Meli Tanzania (TASHICO), Abdulrahman Ally, amesema meli hiyo ni kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi nchini.
Amesema, meli hiyo ni mkombozi mkubwa katika kurahisisha usafiri kwa wafanyabiashara pamoja na kuongeza mwingiliano wa wageni kutoka nje ya nchi na kupanua fursa za kibiashara.

Aidha, amesema meli hiyo ilisha safiri safari nane, na wameshafanya tathimini na kubaini kuwapo kwa kazia ya wateja, hasa wanapotumia Bandari ya Mwanza Kusini ambayo ni maalumu kwa ajili ya mizigo, na sasa wapo katika kuvuta subiri ili kuhakikisha wenzo wa usimamizi wa bandari, wanakamilisha bandari yao vizuri, ili meli hiyo ianze safari zake na kupanga ratiba rasmi.
Naye Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA TAN) Edwin Soko, amesema waandishi wa habari wamefanya ziara hiyo kwa lengo la kutembelea miradi ya kimkakati ,ili wawe mabalozi wazuri wa kuitangaza na kuchangiagia ukuaji wa uchumi wa nchi.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464