` UZINDUZI WA MRADI WA TUZO ZA USHINDANI MAZIWA WATHIBITISHA TANZANIA KUENDELEA KUKUBALIKA KIMATAIFA

WANDAMAN HOTEL

UZINDUZI WA MRADI WA TUZO ZA USHINDANI MAZIWA WATHIBITISHA TANZANIA KUENDELEA KUKUBALIKA KIMATAIFA



Uzinduzi wa Mradi wa Tuzo za Ushindani wa Tasnia Himilivu ya Sekta ya Maziwa kupitia ushirikiano kati ya Serikali, Shirika la Heifer International Tanzania na wadau wengine ni kielelezo tosha cha mafanikio ya awamu ya sita katika kuthibitisha kuwa sera na mikakati yake inakubalika kimataifa .

Aidha hilo linadhirisha pia serikali kupitia sera zake imefanikiwa kuvutia ushirikiano wa kimataifa na uwekezaji wenye tija unaolenga kuongeza uzalishaji, kuboresha masoko na kuinua kipato cha wafugaji wadogo nchini.

Mradi huo wa miaka mitatu utatekelezwa katika mikoa ya Iringa, Njombe, Mbeya na Morogoro.

Uzinduzi wa mfumo wa kuwazawadia watoa huduma binafsi kwa matokeo yaliyothibitishwa,ulizinduliwa mjini Dodoma jana na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Ng’wasi Kamani.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo jijini Dodoma, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Ng’wasi Kamani alisema serikali imeamua kushirikiana na wadau bidhaa hiyo yanaendelea kuongezeka. kuanzisha mfumo wa kupima matokeo ya huduma zinazotolewa kwa wafugaji wadogo wa ng’ombe wa maziwa.

Alisema kupitia mfumo huo, watoa huduma katika maeneo ya afya ya mifugo, uhamilishaji, malisho na ushauri wa ufugaji bora watapatiwa zawadi kulingana na matokeo yatakayopatikana.

“Kwa mfano, mtoa huduma ya uhamilishaji akitumia mbegu bora kwa gharama nafuu na ng’ombe akashika mimba na kuthibitishwa, mtoa huduma atapata Dola za Marekani 15 kwa kila ng’ombe. Hata akifanya kwa ng’ombe 100 au 200, malipo yatazingatia matokeo yaliyothibitishwa,” alisema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Heifer International Tanzania, Mark Tsoxo, alibainisha kuwa ushirikiano huo wa kihistoria unaoendana na uzoefu wa miaka 50 wa shirika hilo nchini.

Aidha Msajili wa Bodi ya Maziwa, George Msaja, na Mratibu wa mradi huo, Edna Lusuva, wakisisitiza jinsi mradi utakavyoziba pengo la mahitaji ya lita bilioni 13 za maziwa kwa mwaka dhidi ya uzalishaji wa lita bilioni 3.1, huku mkaguzi huru kutoka PwC, Nelson Msuya, na mfugaji Anna Almas wakipongeza hatua hiyo inayothibitisha uwezo mkubwa wa uongozi wa awamu ya sita katika kuleta maendeleo endelevu kupitia ushirikiano wa kimataifa.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464