Header Ads Widget

KAMANDA WA POLISI MKOA WA SHINYANGA AHITIMISHA BONANZA LA MICHEZO WILAYANI KISHAPU.



Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi Leo amehitimisha bonanza la michezo kwa maveterani wa timu mbalimbali lililofanyika wilayani Kishapu.

Bonanza hilo ambalo lililenga kuhitimisha sherehe za Sabasaba liliandaliwa na Maveterani wa wilaya ya Kishapu chini ya uongozi wa ndugu Sostenes na kufunguliwa hapo Jana tarehe 08/07/2023 na Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mh. Joseph Mkude.

 Timu hizo za Maveterani zilizoweza kushiriki ni pamoja na timu kutoka Shinyanga, Kakola, Kagongwa, Simiyu, Tabora, Musoma na timu mwenyeji ya Kishapu ambapo timu za Kishapu na Shinyanga zilifanikiwa kutinga fainali na Kishapu kufanikiwa kutwaa kombe.

Akiwa anakabidhi kikombe cha ushindi kwa mshindi wa Bonanza hilo, Kamanda Magomi amesema" michezo ni Afya, inaleta umoja na mshikamano.

Aidha,Kamanda Magomi ameihimiza jamii na wana Shinyanga kuipenda michezo ili kuleta mshikamano.

Ameahidi kuendelea kuyatumia mabonanza na matamasha mbalimbali yenye kulenga kuleta mshikamano katika Jamii kwa lengo la kutokomeza uhalifu mkoani Shinyanga.

Bonanza hilo pia limehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali wakiwemo Mbunge wa Kishapu Mh. Boniphace Butondo, Mbunge wa viti maalum mkoa wa Shinyanga Mh. Lucy Mayenga pamoja na Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Shinyanga.


Post a Comment

0 Comments