Afisa Miradi wa Shirika la TCRS Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Sanyenge akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na wananchi katika Kijiji cha Ilebelebe, Kata ya Itilima wilayani Kishapu kuhusu namna ya kujiandaa na kukabiliana na majanga, ikiwemo mafuriko yanayoweza kusababishwa na mvua kubwa za El Niño Septemba 24, 2026
Shirika la Tanganyika Christian Refugee Services (TCRS) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga limeendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu namna ya kujiandaa na kukabiliana na majanga, ikiwemo mafuriko yanayoweza kusababishwa na mvua kubwa za El Niño, katika Kijiji cha Ilebelebe, Kata ya Itilima wilayani humo.
Elimu hiyo imetolewa Agosti 24, 2026 katika mkutano wa hadhara na wananchi, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa programu inayolenga kuimarisha uelewa na uwezo wa jamii kuchukua tahadhari na kukabiliana na majanga kabla, wakati na baada ya kutokea.
Afisa Miradi wa TCRS Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Sanyenge, amesema miongoni mwa miradi inayotekelezwa na shirika hilo ni pamoja na kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira, udhibiti wa taka na namna jamii inavyoweza kujiandaa na kukabiliana na athari za mvua kubwa za El Niño.
Amesema programu hiyo inatekelezwa katika Kata 10 zilizobainishwa kuwa katika hatari ya kukumbwa na mafuriko, ambazo ni Itilima, Talaga, Mwaweja, Kiloleli, Bunambiyu, Mwasubi, Kishapu, Maganzo, Mondo na Sekebugoro, huku kipaumbele kikitolewa kwa vijiji vilivyo katika maeneo hatarishi zaidi.
Kwa upande wake, Afisa Mazingira wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Charles Kanankabo, amewataka wananchi kuendelea kutunza mazingira kwa kuhakikisha taka zinakusanywa na kutupwa katika maeneo sahihi, pamoja na kuepuka kuziba mifereji na njia za maji, jambo linaloweza kuongeza hatari ya mafuriko wakati wa mvua kubwa.
Mratibu wa Maafa wa Halmashauri hiyo, Robert Mhina, amesema Serikali imeendelea kujiandaa kukabiliana na athari za majanga kwa kuandaa miundombinu na mazingira salama yatakayosaidia wananchi wakati wa dharura, huku akiwataka wananchi wanaoishi katika maeneo hatarishi zaidi kuanza kutafuta maeneo salama kwa ajili ya kujihifadhi pindi hali ya hewa itakapobadilika.
Mhina pia amewataka wafugaji kuchukua tahadhari mapema kwa kuhakikisha mifugo yao inapelekwa katika maeneo salama ambayo hayako katika hatari ya kukumbwa na mafuriko, akisisitiza umuhimu wa wananchi kutumia elimu wanayopewa na kufuatilia taarifa za tahadhari zinazotolewa na mamlaka husika.
Ameongeza kuwa Serikali kupitia Idara za Elimu ya Msingi na Sekondari imeandaa mazingira rafiki na salama kwa wanafunzi, hususani walioko madalasa ya mitihani, ili kuhakikisha mabadiliko ya hali ya hewa hayaathiri ufanyaji wa mitihani na usalama wa wanafunzi.
Naye Mratibu wa Hali ya Hewa wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Deus Gomba, amewataka wananchi kufuatilia kwa karibu taarifa na tahadhari za hali ya hewa zinazotolewa na mamlaka husika, ili waweze kuchukua hatua mapema na kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza.
Amesema ufuatiliaji wa taarifa hizo utawasaidia wananchi kuchukua hatua mapema, kujiandaa na kulinda maisha, mali na mifugo yao dhidi ya madhara yanayoweza kujitokeza, akisisitiza kuwa taarifa ya mapema ni hatua muhimu katika kuzuia madhara ya majanga.
Baadhi ya wananchi walioshiriki mkutano huo wamepongeza juhudi zinazofanywa na Serikali kwa kushirikiana na mashirika kama TCRS katika kuwapatia elimu ya namna ya kujikinga na kukabiliana na athari za majanga.
Christa Christiana, amesema elimu hiyo ni muhimu, hasa kwa wanawake na watoto ambao wanaweza kuathirika zaidi wakati wa majanga, akisema ataendelea kuwahamasisha wanawake wenzake kuchukua tahadhari, kujiandaa mapema na kuhakikisha watoto hawawekwi katika mazingira hatarishi.
Kwa upande wake,Ibrahimu Mhenga amesema elimu hiyo itawasaidia wananchi kujikinga na hatari mbalimbali zinazoweza kujitokeza wakati wa mvua, ikiwemo kuchukua tahadhari wanapoona nyaya za umeme zikiwa zimeanguka chini, huku akiwahimiza wananchi kuhakikisha wanahifadhi chakula cha kutosha kwa ajili ya matumizi wakati wa dharura kama walivyoelekezwa.
Afisa Mazingira wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Charles Kanankabo akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na wananchi katika Kijiji cha Ilebelebe, Kata ya Itilima wilayani Kishapu kuhusu namna ya kujiandaa na kukabiliana na majanga, ikiwemo mafuriko yanayoweza kusababishwa na mvua kubwa za El Niño Septemba 24, 2026
Mratibu wa Maafa wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga , Robert Mhina akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na wananchi katika Kijiji cha Ilebelebe, Kata ya Itilima wilayani Kishapu kuhusu namna ya kujiandaa na kukabiliana na majanga, ikiwemo mafuriko yanayoweza kusababishwa na mvua kubwa za El Niño Septemba 24, 2026
Mratibu wa Hali ya Hewa wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Deus Gomba, akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na wananchi katika Kijiji cha Ilebelebe, Kata ya Itilima wilayani Kishapu kuhusu namna ya kujiandaa na kukabiliana na majanga, ikiwemo mafuriko yanayoweza kusababishwa na mvua kubwa za El Niño Septemba 24, 2026
Afisa Mazingira wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Cassim Said akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na wananchi katika Kijiji cha Ilebelebe, Kata ya Itilima wilayani Kishapu kuhusu namna ya kujiandaa na kukabiliana na majanga, ikiwemo mafuriko yanayoweza kusababishwa na mvua kubwa za El Niño Septemba 24, 2026
Mwakilishi wa Mtendaji wa Kijiji cha Ilebelebe, Kata ya Itilima wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Amos Charles akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na wananchi katika Kijiji cha kuhusu namna ya kujiandaa na kukabiliana na majanga, ikiwemo mafuriko yanayoweza kusababishwa na mvua kubwa za El Niño Septemba 24, 2026
Mwananchi wa Kijiji cha Ilebelebe Kata ya Itilima wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Christa Christian
Mwananchi wa Kijiji cha Ilebelebe Kata ya Itilima wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Suzan Jonh
Mwananchi wa Kijiji cha Ilebelebe Kata ya Itilima wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Hamis Rashidi
Mwananchi wa Kijiji cha Ilebelebe Kata ya Itilima wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Ibrahimu Mhenga
Mwananchi wa Kijiji cha Ilebelebe Kata ya Itilima wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Nzwalu Bundala
Mwananchi wa Kijiji cha Ilebelebe Kata ya Itilima wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Idd Makoye
Mwananchi wa Kijiji cha Ilebelebe Kata ya Itilima wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Alon Dotto