` MAMIA WAMUAGA MAMA WA MHANDISI JAMES JUMBE SHINYANGA

WANDAMAN HOTEL

MAMIA WAMUAGA MAMA WA MHANDISI JAMES JUMBE SHINYANGA

   Mazishi ya marehemu Magreth Limbe Mwinula, mama mzazi wa Mhandisi James Jumbe Wiswa, Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, yamefanyika Jumatano, Juni 10, 2026 katika eneo la Mwasele-Matenkini mkoani Shinyanga.


Ibada ya kuuaga mwili wa marehemu ilifanyika katika Kanisa Katoliki la Moyo Safi wa Maria, Shinyanga Mjini, ambapo ndugu, jamaa, marafiki na waombolezaji mbalimbali walipata fursa ya kutoa heshima zao za mwisho.

Baada ya ibada hiyo, mwili wa marehemu ulisafirishwa kwenda eneo la Mwasele-Matenkini kwa ajili ya maziko.

Mamia ya waombolezaji, wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa dini, ndugu, jamaa na marafiki walihudhuria mazishi hayo na kushiriki kumuaga marehemu katika safari yake ya mwisho.

Marehemu Magreth Limbe Mwinula alifariki dunia Juni 4, 2026 akiwa na umri wa miaka 66. Alizaliwa Desemba 24, 1959 katika Kijiji cha Lugulu, Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu na kubatizwa mwaka 1969.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina.








Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464