` DC MTATIRO AENDESHA KLINIKI YA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI

WANDAMAN HOTEL

DC MTATIRO AENDESHA KLINIKI YA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI

 


DC MTATIRO AENDESHA KLINIKI YA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro, ameendesha kliniki maalumu ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika Tarafa ya Samuye wilayani humo, huku migogoro ya ardhi ikitawala malalamiko yaliyowasilishwa na wakazi walioiomba serikali kuingilia kati ili kurejesha amani na kumaliza migogoro iliyodumu kwa miaka mingi.

TAZAMA VIDEO👇👇
Kliniki hiyo imefanyika leo Juni 11, 2026 katika viwanja vya Shule ya Msingi Usanda wilayani Shinyanga, ambapo wananchi waliwasilisha kero mbalimbali, nyingi zikiwa zinahusu migogoro ya umiliki wa ardhi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wananchi hao wamesema migogoro hiyo imekuwa chanzo cha taharuki, ikiwamo kutishiana maisha, na hivyo kuiomba serikali kuchukua hatua za haraka kuipatia ufumbuzi.
Mmoja wa wananchi hao Nkono Mswagi, amesema alinunua shamba ambalo limeendelea kuwa kwenye mgogoro kwa zaidi ya miaka nane kutokana na kutokuwepo kwa mwafaka kati ya wahusika.

“Tulinunua shamba hili lakini hadi sasa limeendelea kuwa na mgogoro kwa zaidi ya miaka minane, tunaomba serikali itusaidie kutatua suala hili ili tupate haki na kuishi kwa amani,” amesema Mswagi.
Akizungumza wakati wa kusikiliza kero hizo, Mtatiro amewataka watendaji wa vitongoji, vijiji na kata kuacha kupeleka migogoro ya ardhi kwenye mabaraza ya usuluhishi ya kata bila kupata idhini ya Mkuu wa Wilaya.

Amesema baadhi ya migogoro hiyo inaweza kutatuliwa katika ngazi za chini bila kufikishwa kwenye mabaraza hayo, hatua ambayo itasaidia kupunguza ucheleweshaji wa haki na kuongeza ufanisi katika utatuzi wa migogoro.

Aidha, ametoa maelekezo pia kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, kuchakata migogoro yote ambayo imewasilishwa kwenye mkutano huo, na kwamba ndani ya siku 14 wampatie majibu ya utatuzi wake.

TAZAMA PICHA👇👇
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro akizungumza kwenye kliniki ya utatuzi wa kero za wananchi Tarafa ya Samuye.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro akizungumza kwenye kliniki ya utatuzi wa kero za wananchi Tarafa ya Samuye.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro akizungumza kwenye kliniki ya utatuzi wa kero za wananchi Tarafa ya Samuye.
Mwananchi akiwasilisha kero.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464