Wazazi waitwa kuwapeleka watoto wao shule ya hope conscious ambayo inafanya vizuri kitaaluma
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
Mkurugenzi wa shule ya Hope Conscious Pre and Primary School David Moses iliyopo maeneo ya Busongo Kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga, ametoa rai kwa wazazi kuwapeleka watoto wao katika shule hiyo, ambayo imekuwa ikifanya vizuri kitaaluma ili watimize ndoto zao.
Ametoa rai hiyo jana wakati wa hafla ya kusherehekea miaka mitano tangu kuanzishwa kwa shule hiyo.
Amesema shule hiyo, imekuwa ikifanya vizuri kitaaluma, ambapo katika matokeo ya mtihani wa darasa la nne, wanafunzi wao wote walipata ufaulu daraja “B+” ambao ndiyo mtihani wao wa kwanza tangu shule hiyo ianzishwe, huku malengo yao ni kupata daraja “A”. tu kwa mitahini yote.
“nawaomba wazazi walete watoto wao katika shule yetu hii ya Hope Conscious Pre and Primary School ipo maeneo ya Busongo Kata ya Kizumbi, ili wapate elimu bora yenye viwango vya juu na kuyafikia malengo yao,” amesema Moses.
Aidha, ametaja mikakati ya shule hiyo, kwamba licha ya kutoa elimu ya darasani, pia wataanzisha shughuli za ufugaji, bustani, kutengeneza sabauni, viatu, kuanzisha maabara ya utafiti na ubunifu ili kukuza stad za watoto, kufundisha watoto kuandika hadithi na vitabu na kwamba shule hiyo imesajili kama shule ya kibunifu.
Amesema, pia wanatarajia kuanzisha program ya hesabu na mauzo, na kwamba shule hiyo hua wanafanya utafiti wa ndani na nje, na maono ya shule hiyo ni ngazi ya chuo kikuu, kuwa mzazi akipeleka mtoto wake hapo atafurahia matunda yake.
Aidha, ametaja changamoto za maeneo hayo ya Busongo mahali ilipo shule hiyo kuwa wanakabiliwa na ubovu mkubwa wa barabara, pamoja na ukosefu wa huduma ya umeme, na kuomba serikali iwatatulie changamoto hizo.
Nayo risala ya shule hiyo iliyosomwa na Mwanafunzi Brayson Marco, wamesema shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 82 , wasichana 52 na wavulana 30, na kwamba imekuwa ikifanya vizuri kitaaluma.
Naye Mgeni Rasmi Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga Salome Komba, akimwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Alixius Kagunze, ameipongeza shule hiyo kwa kufanya vizuri kitaaluma, huku akiwasihi wazazi kuwapeleka watoto wao shule ambao wamefikia umri wa kuanza masomo katika mwaka mpya wa masomo 2026.
Amesema, amefurahishwa na shule hiyo namna inavyopanga mipango yake ya baadae katika kufundisha watoto vitu vya ziada, ilikiwamo somo la hesabu na mauzo, kwamba watoto watafundishwa elimu ya ujasiriamali na biashara na wakihitimu darasa la saba watakuwa na ujuzi mkubwa.
Amewata pia wazazi, kufutalia maendeleo ya watoto wao wanapotoka shule ikiwamo kukagua kazi za nyumbani ili kutoa ushirikiano kwa walimu na kufanya vizuri kitaaluma.
Akijibu changamoto ambazo zinaikabili shule hiyo na eneo zima la Busongo, kuwa na ubovu wa miundombinu ya barabara ba ukosefu wa umeme, kwamba amelichukua na watalifanyia kazi kwa kufikisha kwa mamlaka husika Tanesco na Tarura ili zipate kutatuliwa haraka.
Katika hafla hiyo pia ilikatwa kake kwa ajili ya kuashiria ufunguzi rasmi wa shule hiyo pamoja na kupata usajili rasmi 15.1.2025 na kuwashukuru wadau mbalimbali ambao wamewaunga mkono kutoka ndani ya nchi na nje ya nchi.
TAZAMA PICHA👇
Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga Salome Komba akizungumza.
Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga Salome Komba akizungumza.
Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga Salome Komba akizungumza.
Mkurugenzi wa shule ya Hope Conscious Pre and Primary School David Moses akizungumza.
Mkurugenzi wa shule ya Hope Conscious Pre and Primary School David Moses akizungumza.
Mwanafunzi wakisoma risala ya shule.
Muonekano wa shule.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464