` WANAWAKE WAWILI WAFARIKI DUNIA KWA KUFUKIWA NA KIFUSI SHINYANGA

WANAWAKE WAWILI WAFARIKI DUNIA KWA KUFUKIWA NA KIFUSI SHINYANGA




Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi 

Suzy Butondo Shinyangapressblog 

Wanawake wawili wa  Kitongoji cha Itwili Kata  na Tarafa ya Old Shinyanga Mkoani  Shinyanga ,wamefariki dunia baada ya kufukiwa na kifusi cha udongo  kwenye shimo wakati wakitoa mawe kwaajili ya kuponda kokoto. 

Akinzungumza na Vyombo vya Habari Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi amesema wamepata taarifa za tukio hilo majira ya saanne asubuhi na kwamba mmoja wa marehemu hao anatambulika kwa jina la Suzana Samweli (41) huku mwingine akijulikana kwa jina la Hapnesi Peter (20).

Akielezea tukio hilo Kamanda Magomi amesema chanzo cha tukio  ni kutochukua tahadhali   mapema wakati wakitekeleza  shughuli  yao ya kuponda kokoto.

Aidha Kamanda Magomi amesema miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga kwaajili ya taratibu za uchunguzi huku akiwaomba Wananchi kuchukua tahadhali kabla ya kutekeleza majukumu yao ili kuimarisha usalama wao na walipo eneo hilo.

Mwenyekiti wa kijiji cha Old Shinyanga  Dotto Bwile amesema kweli tukio hili limetokea toka asubuhi saa nne walikuwa wakiponda mawe kwa ajili ya biashara,  ambayo ni shughuli yao ya kila siku

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464