` CCM SHINYANGA YAPONGEZA HOTUBA YA RAIS NA KUWASIHI WANANCHI KUÀCHA KUANDAMANA ILI KUEPUSHA MATESO KWA WANANCHI

WANDAMAN HOTEL

CCM SHINYANGA YAPONGEZA HOTUBA YA RAIS NA KUWASIHI WANANCHI KUÀCHA KUANDAMANA ILI KUEPUSHA MATESO KWA WANANCHI


Katibu wa siasa na uenezi wa chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Shinyanga Richard Masele

Suzy Butondo,Shinyangapress blog

Katibu wa Siasa na uenezi  wa chama Cha Mapinduzi CCM mkoa wa Shinyanga Richard Masele  amewasihi wananchi wa mkoa wa Shinyanga waache kufanya maandano siku ya tarehe tisa wakae kwa utulivu  na walinde amani ya Tanzania, kwani kufanya hivyo wanaweza kusababisha wazazi na watoto kuteseka.

Pia chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga kimepongeza hotuba ya Rais Samia Suluhu  aliyoitoa tarehe 3/12/2025 ambapo alikemea maandamano, na kuhamasisha uchumi na maendeleo, kutumia rasilimali zilizopo na si kutegemea misaada kutoka nje.
 
Hayo ameyasema leo wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani Shinyanga ofisini kwake , ambapo amesema ili wananchi wasio na hatia wasiteseke ni vizuri kuachana na maandamano ambayo yanaweza kusababisha uvunjifu wa amani ya nchi ya Tanzania.

,Nchi yetu ya Tanzani ni nchi ya amani tusikubali kushawishika tukaingia kwenye maandamano ambayo yanaweza kuleta uvunjifu wa amani yetu, tukasababisha maafa makubwa kwenye nchi yetu, niwaombe vijana wote wa mkoa wa Shinyanga ikiwa ni pamoja na watanzania wote siku ya tarehe tisa tukae kwa utulivu ili kuilinda amani yetu,amesema Masele.

,Tukikubali kushawishika  kuandamana wazee wetu, watoto wetu na watanzania wengi watateseka, hivyo niwasihi vijana wenzangu tuendelee kuilinda amani yetu, tukifanya maandamano haya tujue tunawadhuru wazazi wetu  babu zetu zetu, watoto wetu jirani,  tusiandamane tuitunze amani yetu,  hii ni tunu tuliopewa na mwenyezi Mungu  tusiwatese wananchi wenzetu, ameongeza.

,Tuangalie baadhi ya Mataifa yaliyopoteza amani kwa kushinikizwa,walipoteza amani yao wakarudi kuanza kujuta kwa nini walifanya hivyo, niwaombe tumuunge mkono Rais Samia Suluhu Hassan ili aendelee kuleta maendeleo katika nchi ya Tanzani, kwani tayari amefanya maendeleo  makubwa toka aingie madarakani hivyo anastahili kupongezwa , na kumtia moyo tusikubali kujazwa chuki na tukamchukia Rais wetu,amesisitiza.

Amesema kuna baadhi ya watu wanadai katiba mpya wanatakiwa kudai kwa utulivu na kulinda amani,  wasidai kwa kuhamasisha vurugu, katiba ina mchakato wake ambapo Rais hajakataa itafanyiwa kazi kwa utulivu sio kwa vurugu ambayo inasababishwa na watu wachache ambao hawapendi tudumishe amani yetu wanataka tuebdelee kuvurugana.

,Tukumbuke maandamano yaliyotokea siku za uchaguzi yamesababisha baadhi ya vifo vya watu, mali za watu kuteketezwa na kuibiwa,hivyo tukatae kwa kulinda amani yetu tusikubali kushawishiwa na watu ambao wanaishi nje ya nchi yetu sisi sote tuhurumiane,

Masele amesema anaungana na mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM mkoa Mabala Mlolwa kuwapa pole ndugu wa marehemu waliopoteza wapendwa wao na Mungu awalaze mahali peponi wapumzike kwa amani.

,Niwasihi tuendelee kuchapa kazi ili nchi yetu kwa kusimiamiwa na chama cha Mapinduzi CCM iendelee kuleta maendeleo makubwa, ambapo katika sekta ya afya, Umeme, elimu na miundombinu ya barabara tayari kuna mabadiliko makubwa , na pia niwaombe vijana wote mkae mkao wa kuchapa kazi, serikali imejipanga vizuri  kuwapatia mikopo vijana, wanawake na watu wenye ulemavu ili muweze kujikwamua kiuchumi, amesema 













Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464