
Wanawake wa Tanzania, kupitia UWT Taifa na Mwenyekiti Mary Chatanda, wametangaza rasmi makubaliano muhimu yenye vifungu vinavyolenga kuimarisha amani nchini.
Wito wao mkubwa ni kwa wanawake wote kudumisha upendo, heshima, mazungumzo na kusameheana.
Msimamo wa Wanawake: Wanawake wameahidi kuiheshimu, kuitunza, na kuimarisha amani ya Tanzania. Wanasisitiza kuwa hakuna maendeleo yatakayopatikana bila amani, na ndiyo maana wanapinga aina zote za rushwa na migogoro mikubwa na midogo inayohatarisha utulivu.
Kukataa Vurugu na Upotoshaji: Azimio hili linakataa vikali vitendo vya ukosefu wa amani, udhalilishaji, unyanyasaji wa kijinsia, ubakaji, ukatili, pamoja na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii yanayosababisha chuki na mifarakano.
Wameahidi kupinga taarifa potofu, lugha za chuki na kazi zinazoleta mpasuko katika jamii. Ushirikiano na Malezi Bora: Wanawake wamejitolea kuimarisha ushirikiano katika familia na jamii nzima ili kulinda mshikamano.
Pia, wameahidi kuendeleza malezi mazuri na mienendo mwema kwa watoto na vijana ili kukataa utamaduni wa kusikiliza sauti za mitandaoni zinazochochea chuki.
Ujumbe kwa Vijana: Mary Chatanda amewataka vijana waache kutumika kwa maslahi ya kisiasa. Ametoa wito kuwa makini na kinachoendelea katika mitandao na kujiepusha nayo kwa maslahi mapana ya taifa.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464