` USHIRIKIANO NA VIONGOZI WA DINI WATAJWA KAMA NGUZO YA KULINDA AMANI NCHINI

USHIRIKIANO NA VIONGOZI WA DINI WATAJWA KAMA NGUZO YA KULINDA AMANI NCHINI


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema serikali imeendelea kufanya mikutano na viongozi wa taasisi mbalimbali za dini, ikiwemo Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), na viongozi wa kimila ili kuwaeleza hali halisi ya usalama nchini na kuwataka kuendelea kudumisha amani.

Kauli hiyo aliitoa wakati akizungumza na wananchi wa Arusha katika ziara byake ya kikazi ambayo poia ameitumia kuangalia uharibifu uliofanywa katika vurugu ya Oktoba 29.

Waziri Mkuu amesisitiza umuhimu wa amani kama msingi mkuu wa maendeleo ya taifa.

Katika ziara hiyo pia aliwapa wananchi salamu za pole zilizotolewa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kufuatia athari za vurugu zilizotokea hivi karibuni.

Waziri Mkuu alitembelea na kukagua uharibifu uliotokea wakati wa vurugu za Oktoba 29, 2025, ambapo Kituo cha Polisi cha Kikatiti, Mahakama ya Mwanzo ya Maji ya Chai, na kituo cha mafuta cha Total Energies vilichomwa moto. Aidha, alibaini kuibwa kwa mali katika soko kuu na kubomolewa kwa sefu ya kutunzia fedha.

Waziri Mkuu amewaonya wananchi kuwa kuchagua vurugu ni sawa na kuchagua kufukuza maendeleo na kuongeza umaskini kwa mtu mmoja mmoja, akisisitiza kuwa ahadi za maendeleo kama maji na barabara zitafanyika endapo tu nchi itakuwa na aman
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464