
Moja ya matunda ya wazi ni uimarishaji wa usafiri katika maziwa makuu. Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) hivi karibuni limeripoti mafanikio makubwa katika Bandari ya Karema, Ziwa Tanganyika.Meli mbili za mizigo zenye uwezo wa kubeba tani 2,000 kila moja zimeingizwa majini. Hii ni hatua kubwa itakayochochea biashara kati ya Tanzania, Kongo (DRC), na Burundi.
Miradi hii si tu inarahisisha usafiri, bali inazalisha ajira kwa vijana na kukuza uchumi wa mikoa ya pembezoni kama Katavi na Kigoma.
Chini ya uongozi wa Rais Samia, Serikali imejielekeza katika kutekeleza Ilani kwa vitendo, ikilenga kufikia malengo ya Dira ya Taifa 2050 kwa kuhakikisha inaweka mazingira ya uwekezaji sawa kupitia diplomasia ya kiuchumi. Kwa sasa, Tanzania imekuwa kivutio kikubwa kwa wawekezaji wa kimataifa (kama ilivyoonekana kwenye mradi wa meli wa Karema), jambo linaloongeza mzunguko wa fedha na kukuza viwanda.
Aidha ujenzi wa miundombinu ya barabara, reli (SGR), na nishati ya umeme ni sehemu ya mkakati wa kuhakikisha kila Mtanzania anafurahia matunda ya uhuru.
Kwa mujibu wa viongozi wa kiroho na wananchi wazalendo, matunda haya yataendelea kuwa na maana kwa watanzania ikiwa hawatakubali kuingiza uanaharakati au uchochezi wa maandamano katika mambo ya msingi ya nchi.
Kauli mbiu ya #Hatuandamani imekuwa kielelezo cha utambuzi wa wananchi kuwa maendeleo yanahitaji utulivu, si fujo.Katika hili Wananchi wanahimizwa kuendelea kuwa na imani na Serikali kwani nia yake ni njema na malengo yake ni makubwa kwa ustawi wa wote.
"Usambazaji wa taarifa sahihi unalinda jamii dhidi ya uvumi na hofu. Tuandike historia ya nchi yetu kwa kufanya kazi, si kwa kupiga kelele za uanaharakati zinazodidimiza uchumi."
Tanzania inaelekea katika hatua nyingine kubwa ya kimaendeleo. Kazi ya kuwezesha maendeleo chini ya Rais Samia ni jukumu la kila mwananchi kwa kulinda amani, kufanya kazi kwa bidii, na kupuuza mianya yote ya uanaharakati inayolenga kuvuruga utekelezaji wa mipango ya Taifa.
Mabadiliko ya Kiuchumi Katika Bandari ya Karema, kutoka kuwa na uwezo mdogo wa kuhudumia mizigo mikubwa na usafirishaji ambao ulitegemea vyombo vidogo ambavyo vilichelewesha biashara na kuongeza gharama za usafirishaji kwa wafanyabiashara wa mkoa wa Katavi na maeneo ya jirani. hadi kupata meli kubwa sasa ni hatua ambayo si tu italenda maendeleo lakini kuwezesha mzunguko wa fedha kuwa mkubwa.
Kwa uwekezaji huu wa Serikali ya Awamu ya Sita, taswira ya kiuchumi ya Karema inaenda badilika na kuwa lango kuu la biashara ya kimataifa. Uwepo wa meli hizi sasa unatoa uhakika wa usafirishaji wa bidhaa kwa wingi na kwa haraka, jambo linalofungua soko la kudumu kati ya Tanzania na nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Burundi. Hii inamaanisha kuwa gharama za bidhaa zinapungua kwa mlaji wa kawaida na faida inaongezeka kwa mfanyabiashara, huku Bandari ya Karema ikigeuka kuwa kitovu cha ajira rasmi na zisizo rasmi kwa wakazi wa mkoa huo.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464