` “HATUKUBALI UDINI WALA VURUGU”: WANANCHI WAKEMEA MPANGO MPYA WA WACHOCHEZI

“HATUKUBALI UDINI WALA VURUGU”: WANANCHI WAKEMEA MPANGO MPYA WA WACHOCHEZI


Watanzania wameanza kuweka wazi hofu yao kuhusu njama mpya za uchochezi zilizopangwa na baadhi ya watu nchini na nje ya nchi baada ya mipango yao ya vurugu kushindwa kufua dafu mnamo Desemba 9. Kwa sasa, taarifa zinazosambaa mtandaoni zinaashiria kuwa wachochezi hao wanapanga kutumia fursa ya Sikukuu ya Krismasi, Desemba 25, kwa ajili ya kutekeleza makusudi yao.

Mijadala mingi katika mitandao ya kijamii inaonyesha wananchi wengi wamejitokeza kukemea vikali mipango hiyo na kutoa wito kwa umma kuendelea kufanya mambo yao kwa kufuata itikafi za usalama na kutoshirikiana na watu wenye nia ovu.

Kukataa Udini na Maandamano ya Vurugu

Moja ya hoja kuu inayoelekezwa dhidi ya wachochezi hao ni jaribio la kubadilisha ajenda yao ya vurugu na kuifanya ionekane kama suala la kidini. Hili linakuja baada ya wachochezi, akiwemo Mange Kimambi anayeishi nje ya nchi, kuonekana kushindwa kuhamasisha umma mnamo Desemba 9.

"Pazaaa sautii baba.... InshaAllah tunataka Amani hatutaki udini. Nchi yetu ya Amani Mungu aitunzee🙏," alisema mmoja wa wachangiaji, akisisitiza kuwa wananchi hawataki udini wala migawanyiko.

Wito umesisitizwa: "Kataa maandamano, dumisha amani ya nchi yetu".

Ushindi wa Desemba 9 na Mwendelezo wa Njama

Wananchi wengi wamepongeza umoja na busara iliyotumiwa na Watanzania ambayo ilisababisha kushindwa kwa jaribio la vurugu mnamo Desemba 9. Wengi wanaamini kuwa vijana wameshaanza kushtukia na kutambua malengo halisi ya wachochezi hao.

"Wanao jielewa wote wamesha mshtukia🙌🙌," alisema mmoja wa wananchi.

Hata hivyo, wito umetolewa kwa vijana waendelee kuwa macho dhidi ya njama za Desemba 25, ambapo wachochezi wanajaribu kutumia fursa ya Krismasi kuvuruga amani.

Wito wa Umoja Kazi ya Kuielimisha Jamii

Kutokana na hali hiyo, baadhi ya raia wenye sauti kubwa, kama yule aliyefahamika kwa jina la mtandaoni kama @zungu_kakere_og, wamepongezwa na kuombwa kuongeza juhudi za kuelimisha vijana dhidi ya propaganda.

"Mungu atakulipa kaka, azidi kukupa nguvu," alisema mmoja wa wafuasi. Wito umetolewa pia kwa vijana wengine wa kizalendo kujiunga na kupaza sauti ili kupambana na nguvu ya ushawishi ya wachochezi wanaojaribu kuhamasisha vurugu kupitia wingi wa taarifa za uongo.

Wananchi wamehimizwa kutokubali kuchonganishwa na Serikali yao na kutambua kuwa usalama wa Taifa ni kipaumbele cha kila Mtanzania. 

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464