` RC MHITA ATAKA HUDUMA BORA YA UMEME KWA WANANCHI,AKIMKARIBISHA MENEJA MPYA WA TANESCO MKOA WA SHINYANGA

RC MHITA ATAKA HUDUMA BORA YA UMEME KWA WANANCHI,AKIMKARIBISHA MENEJA MPYA WA TANESCO MKOA WA SHINYANGA



Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita, amelitaka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Shinyanga, kutoa huduma bora kwa wananchi, pamoja na kuwapatia taarifa pale wanapokuwa wakifanya maboresho ya miundombinu yao na siyo kukata umeme ghafla.
Mhita amebainisha hayo leo Desemba 17,2025 wakati akimkaribisha Meneja Mpya wa TANESCO Mkoani humo, Mhandisi Hadija Mbaruku, alipowasili rasmi kujitambulisha ofisini kwake.

Amesema, Shirika la Umeme, linafanya kazi nzuri ya kuboresha miundombinu ya umeme, lakini limekuwa likikabiliwa na changamoto ya utoaji wa taarifa kwa wananchi pale linapofanya maboresho ya miundombinu hiyo, na kukata umeme ghafla na kuathiri shughuli za kiuchumi kwa wananchi ikiwamo uzalishaji mali.
“karibu sana Meneja mpya wa TANESCO hapa mkoani Shinyanga, maelekezo ya Serikali chini ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan, ni kutoa huduma bora kwa wananchi,”amesema Mhita.

Aidha, amesisitiza kwamba waboreshe zaidi kitengo chao cha mawasiliano na kutoa taarifa kwa wananchi wakati wa maboresho hayo ya miundombinu, ili wananchi wajiandae mapema kuweka ratiba zao vizuri kabla ya umeme kukatika na kutoa athiri shughuli zao za kiuchumi na tabia hiyo ipo sana katika wilaya ya Kahama.
“”Information is power” mnapotoa taarifa mapema mnakuwa pia na mahusiano mzuri kati ya wananchi na shirika,”amesema Mhita.

Pia, ametoa maelekezo kwa shirika hilo kutoa elimu kwa wananchi juu ya matumizi sahihi ya umeme, pamoja na kutumia mafundi waliothibitishwa na TANESCO kufunga mifumo ya umeme majumbani mwao ili kuepuka hitilafu za umeme na kusababisha nyumba zao kuungua.
Amewapongeza pia, kuwa na dawati la Malalamiko la kupokea kero za wananchi pamoja na kufuatilia kero hizo na kuzitatua mara moja na kwamba utatuzi wa kero hizo kwa wakati ni kuleta faraja kwa wananchi.

Naye Meneja mpya wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Hadija Mbaruku, ameshukuru kwa mapokezi mazuri, na kwamba maelekezo yote atayafanyia kazi, ikiwamo kuboresha huduma bora kwa wananchi.
Amesema, maboresha ya huduma ya umeme, yatamatika Desemba 23, na kwamba maelekezo waliyopewa sikukuu za mwisho wa mwaka, wananchi washerehekee bila umeme kukatika.

TAZAMA PICHA👇👇
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita akizungumza na Meneja mpya wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Hadija Mbaruku.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita akizungumza na Meneja mpya wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Hadija Mbaruku.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita akizungumza na Meneja mpya wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Hadija Mbaruku.
Meneja mpya wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Hadija Mbaruku akizungumza.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita (kushoto)akimkaribisha Meneja mpya wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Hadija Mbaruku ofisini kwake.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita (kushoto)akimkaribisha Meneja mpya wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Hadija Mbaruku ofisini kwake.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464