` BAADHI YA WAUMINI WAKATOLIKI WAPINGA MAHUBIRI YA RUWA’ICHI,WASEMA KANISA SIO MTU MMOJA

BAADHI YA WAUMINI WAKATOLIKI WAPINGA MAHUBIRI YA RUWA’ICHI,WASEMA KANISA SIO MTU MMOJA


Na Mwandishi Wetu

Baadhi ya Waumini wa Kanisa Katoliki Mkoa wa Dae es Salaam kupinga kauli za Askofu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Jude Thaddeus Rawai'chi ya kusema lofa”, “mpumbavu”, “njaa njaa”, “msaliti” kwa kutumia madhabahu haikuwa sawa.

Waumini wamesema kuwa kama waumini waliopeleka Barua kwa ubalozi wa Vatiican kulikuwa hakuna sababu ya kutumia madhabahu badala yake wangeitwa faragha kutokana maandiko yalivyotaka.

Wakizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Waumini, Mackdeo Shilinde na Gerald Abel  wamesema kauli ya   Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Jude Thaddaeus  Ruwa’ichi kugeuza  mimbari kuwa  jukwaa la  hukumu na vitisho haikuwa sawa na  badala yake alitakiwa kuinjilisha  Injili ya mapendo na umoja.

Katika tamko lao, waumini hao wamesema kuwa kupitia kauli zake wanataka Askofu  Kanisa kuendeshwa kwa misingi na inapotokea changamoto kwa waumini basi kuwepo na utatuzi unaokwenda kujenga na sio kugombana kwa kwa kutumia mimbari


Shillinde amessema  kuwa Kanisa si mali ya Askofu wala Padri mmoja, bali ni jumuiya ya waumini wakatoliki.

Shillinde amesema Matusi Madhabauni yanazua haasira za  waumini kwa maneno mazito kama “lofa”, “mpumbavu”, “njaa njaa”, “msaliti” na “ndumilakuwili” — kauli walizosema zinakiuka moja kwa moja mafundisho ya Biblia.

Waumini hao wamenukuu wazi Maandiko Matakatifu yanayokataza hukumu na udhalilishaji, wakisema "Msihukumu, msije mkahukumiwa.” (Mathayo 7:1)" yakifuatia na kufungu kingine cha  “Usimhukumu mtumishi wa mtu mwingine.” (Warumi 14:4)"“Neno lenu na liwe daima na neema.” (Wakolosai 4:6)"

Kwa mujibu wa waumini, hakuna sehemu ya Biblia inayoruhusu kiongozi wa dini kuwaita waumini wake majina ya kudhalilisha hadharani, hasa kutoka madhabauni.

Katika msimamo wao, waumini hao wamesisitiza kuwa mimbari imewekwa kwa ajili ya kuunganisha waumini na kuwafariji, si kuwadhalilisha. Wamenukuu pia “Heri wapatanishi, maana hao wataitwa wana wa Mungu.” (Mathayo 5:9) “Jitahidini kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha amani.” (Waefeso 4:3)"

Shilline amesema kauli za matusi kutoka madhabauni zinawakwaza waumini, kinyume na onyo la Biblia linalosema:

“Msiwakwaze wadogo hawa.” (Mathayo 18:6)"

Shilinde na Abel wamesema kauli hizo hazikujibu hata hoja moja kati ya zile zilizowasilishwa kwa mamlaka za juu za Kanisa kupitia barua ya waumini Stanslaus Nyakunga na Elia Phaustine kwa Balozi wa Vatican.

Wamesema Barua hiyo iliomba tathmini ya mwenendo wa Padri Charles Kitima, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), anayelalamikiwa kuhusishwa na siasa 

Shillinde amesema  badala ya hoja kujibiwa kwa busara au kufanyiwa uchunguzi wa kikanisa, walishuhudia waumini wakiburuzwa hadharani kwa maneno ya dharau.

Waumini hao wamesema  kwamba Kanisa Katoliki halipaswi kuingizwa katika siasa za chama chochote, wakisisitiza kuwa Padri au Askofu anapaswa kuwa muunganishi wa waumini na Taifa, si mshauri wa chama cha siasa.

Amesema Padri si Kanisa, Askofu si Kanisa , Kanisa ni waumini wakiongeza kuwa Kanisa linapaswa kuwa kimbilio la wote, si kumbatio la wachache wenye sauti au mamlaka.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464