` TANZANIA NI SALAMA,MAISHA YANAENDELEA:WAFANYABIASHARA WADOGO WAREJEA KWENYE HALI YA KAWAIDA

TANZANIA NI SALAMA,MAISHA YANAENDELEA:WAFANYABIASHARA WADOGO WAREJEA KWENYE HALI YA KAWAIDA

Tanzania Ni Salama, Maisha Yanaendelea: Wafanyabiashara Wadogo Warejea Kwenye Hali ya Kawaida


Baada ya siku chache za changamoto, wafanyabiashara wadogo kote nchini wameanza kurejesha shughuli zao za kila siku, wakithibitisha utulivu na uthabiti wa Tanzania kama nchi salama. Hali hii inarejesha imani kwa wananchi na wadau wa kimataifa.


Gaspar Apolnary, mfanyabiashara anayetegemea kipato cha siku, alieleza jinsi alivyopata athari kubwa kibiashara kwani hakuweza kufanya kazi kwa siku tano.


 "Kipato chetu cha kawaida tunajitafutia tule, siku unapotoka kidogo unapata chochote kitu unapeleka nyumbani," alisema. Aliongeza kuwa vurugu ilisababisha hofu na kusababisha vitu kupanda bei. Hata hivyo, alieleza matumaini: "Mungu ni mwema kwa sasa hivi tumerejea katika hali yetu ya kawaida, tumerejea."


Shaban Moshi Shaban, dereva pikipiki (bodaboda) wa Kimara Mwisho, alieleza jinsi marufuku ya kutofanya kazi usiku ilivyoathiri biashara yake ambayo hufanywa kwa saa 24. Aidha, alibainisha jinsi baadhi ya bidhaa, kama mafuta, zilivyopanda bei, na kuleta changamoto kubwa ya maisha.


Pamoja na changamoto hizo, Shaban alitoa shukrani kwa juhudi za serikali na vyombo vya ulinzi: "Tunashukuru serikali ilifanya jitihada kubwa imepambana na hili suala. Napenda kulipongeza jeshi la ulinzi limefanya kazi vyema mpaka sasa hivi hakuna changamoto yoyote." Kurejea kwa haraka kwa shughuli za kiuchumi kunathibitisha kuwa Taifa linaendelea kuwa salama na linaelekea kwenye kasi ya maendeleo. 

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464