` UZALENDO NA THAMANI YA TAIFA: AMANI YETU, UTAJIRI WETU

UZALENDO NA THAMANI YA TAIFA: AMANI YETU, UTAJIRI WETU




Wito wa uzalendo wa kweli umepewa kipaumbele, huku wananchi wakikumbushwa kutambua na kuthamini amani na uhuru wao kama msingi wa maisha ya Taifa.


Gaspar Apolnary alikumbusha: "Sisi tumeshazoea nchi yetu ni ya amani, tuko na uhuru kila siku unaenda maeneo yoyote ni salama." Alisisitiza umuhimu wa kuenzi hali hii: "Tukae kwa amani kwa sababu watu wengi wanategemea kutoka kwetu )wafanyabiashara)... na hivi kumwezesha kila mtu kufanya shughuli kwa ajili ya familia yake na taifa."


Shaban Moshi Shaban alieleza kuwa matendo ya vurugu yaliyoonekana si uzalendo, bali ni uhalifu, na kwamba maandamano yanapaswa kubeba ujumbe wazi na wa kisheria. "Kitu wanachokifanya ni kitu ambacho hakifai... waache kufanya hicho walichokuwa wanakifanya kwa sababu ni uhalifu," alisema.


Uzalendo wa kweli unahusisha kujenga, kulinda mali za umma na za watu binafsi, na kuepuka vitendo vinavyovuruga amani na utulivu wa nchi. Kila Mtanzania anahimizwa kudumisha utulivu na kufuata sheria ili kuendeleza maisha yetu katika mazingira ya amani tuliyoyazoea.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464