
🏛️ Wadhifa na Uzoefu Wake wa Uongozi
Amewahi kuwa Naibu Spika wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament) – nafasi iliyompa uzoefu mpana wa uongozi wa kanda na bara.
Amekuwa Mbunge wa Shinyanga Mjini, akisimamia kwa ufanisi miradi ya maendeleo ya wananchi.
Ni mjumbe na kiongozi waandamizi katika Chama Cha Mapinduzi (CCM), akihusika katika kusimamia ajenda za vijana, uchumi na teknolojia.
Amefanya kazi na mashirika ya kimataifa katika masuala ya innovation, digital transformation, na uongozi wa kizazi kipya.
💡 Kwa Nini Stephen Masele?
👉Anaelewa mwelekeo wa dunia ya kisasa na kasi ya mabadiliko ya teknolojia.
👉Ni sauti ya matumaini ya vijana wa Tanzania, mwenye busara, uthubutu, na hekima.
👉Ana uwezo wa kusimamia uwajibikaji wa Serikali kwa lugha ya kizazi cha sasa, yenye uthabiti na maarifa.
👉Anathamini umoja, maendeleo, na heshima kwa kila Mtanzania, bila kujali chama, dini, au asili.
🙏 Uongozi wa Kimungu
Stephen Masele ameunganishwa na imani na uongozi wa kimaadili. Ni kiongozi wa kiroho, mnyenyekevu, mchapakazi, na mzalendo — anayejua kuwa “Leadership is service, not status.” Amebarikiwa kwa neema ya Mungu kumtumikia taifa kwa hekima, uaminifu, na upendo wa kweli.
“Uongozi wa kweli hutoka kwa Mungu, na anayechaguliwa kwa neema yake hutoa nuru kwa watu wake.” (Mithali 11:14)🌍 Wito kwa Waheshimiwa Wabunge
Kwa heshima na taadhima, tuangalie mbele. Tuitazame Tanzania ya leo na ya kesho. Tuchague kiongozi anayeakisi mioyo na matumaini mapya ya Watanzania. Tumpokee Steven Masele — Spika wa Kizazi cha Sasa!
🌟 Mabadiliko ya Bunge Letu ni Sasa! 🌟
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464