` NI MPANGO MCHAFU: NIA NI KUHUJUMU UCHUMI NA MAISHA YA WATANZANIA

NI MPANGO MCHAFU: NIA NI KUHUJUMU UCHUMI NA MAISHA YA WATANZANIA

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amefichua kwamba vurugu za Oktoba 29 hazikuwa tu uharibifu wa mali, bali zilikuwa ni jaribio lililopangwa la kuhujumu na kuua uchumi wa nchi na kudhoofisha maisha ya Watanzania mmojammoja.

Akizungumza kwa hisia, na wahariri na waandfishi wa habari waandamizi jijini Dar es salaam,Dkt. Mwigulu alieleza jinsi wahuni hao walivyolenga miundombinu muhimu:"Mpango uliwekwa pasiwe na miundombinu ya hawa watu kusafiri. Walipanga kuchoma stendi ya mabasi ya Magufuli, kituo cha kuzalisha umeme cha Kinyerezi na reli ya SGR. Hizi siyo mali za Serikali, ni mali za umma," alisema.

Alisisitiza kuwa uharibifu huo uliathiri maisha ya kila siku ya Mtanzania: "Maisha ya Mtanzania mmojammoja yanahusisha mtu kutoka sehemu moja kwenda nyingine ili kujipatia riziki zao. Hawa watu wasipotoka unataka wale nini?"

Dkt. Mwigulu alitumia fursa hiyo kusisitiza kwamba fedha zinazotekeleza miradi mikubwa—kama vituo vya DAWASCO, barabara, na zahanati—si za Serikali, bali ni za Watanzania.

"Ukinunua shati kuna sehemu unapeleka kujenga barabara, unakuwa umetenga sehemu ya kutumia na sehemu umejinyima ili kuchangia maendeleo ya nchi. Hivyo unapochoma kituo cha DAWASCO kinachowapa maji safi na salama, unataka hawa watu waishije?" alihoji Waziri Mkuu, akionyesha jinsi hujuma inavyogusa maisha ya mtu mmoja mmoja.

Aliwataka watanzania kuelewa njama za makusudi zinavyopangwa ili kuvuruga mfumo wa maisha na kudidimiza maendeleo yaliyopatikana nchini. 

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464