
Serikali ya Tanzania imewataka watu na vyombo vya habari kufuata weledi na maadili ya uandishi wa habari, huku ikielekeza kidole kwa wale wanaotumia habari kama silaha ya kupanda chuki na kuvuruga amani.
Hivi karibuni, Mtangazaji wa CNN, Larry Madowo, mwenye asili ya Kenya, amekosolewa vikali na Watanzania kwa kurusha habari kuhusu uchaguzi wa Oktoba 29 (2025) zilizokolezwa chumvi kupita kiasi kwa lengo la kuchafua taswira ya nchi.
Uhasama Kutoka Kenya na Wajibu wa Polisi
Wachambuzi wanasema kuna ongezeko la Watanzania na Wakenya wanaotumia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kulenga kuvunja umoja wa Watanzania, kuwafarakanisha, na kuharibu kasi ya ukuaji wa uchumi, hasa baada ya Tanzania kuipiku Kenya katika uwekezaji, kwa mujibu wa ripoti ya Merchant Bank.
Hali hii inakwenda sambamba na matukio ya hatari, ikiwemo kukamatwa kwa Charles Onkuni Ongeta, Mwanajeshi wa Marekani mwenye asili ya Kenya, kwa jaribio la kuingiza mabomu manne ya CS M68 nchini Tanzania mnamo Novemba 16, 2025.
Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa, amesisitiza kuwa:"Hatuwazuii kufanya kazi yao, lakini wafanye kazi kwa kuzingatia misingi ya uandishi na utangazaji wa habari, wazingatie weledi na maadili," alisisitiza Msigwa, akionya dhidi ya habari kugeuzwa silaha.
Aidha, Serikali inasisitiza kwamba kama mataifa mengine, Tanzania ina haki ya kulinda taifa lake kwa mujibu wa Katiba dhidi ya wale wanaodhamiria kuiangusha serikali, kama ilivyokuwa wakati wa vurugu za uchaguzi.
Mfano wa Marekani:
Katika taifa wanalofanya kazi (Marekani), Polisi wameua raia zaidi ya 11,000 ndani ya miaka 10, hali inayoonyesha kuwa vyombo vya dola vipo tayari kutumia nguvu kulinda amani na usalama.
Mfano wa Kenya:
Katika chaguzi tano nchini Kenya, watu zaidi ya 2,500 walipoteza maisha yao kutokana na vurugu.
Taarifa inahitimisha kwa onyo kwamba wale wanaojitokeza kama "vibarakala wa Mabeberu" kwa ajili ya pesa na kuharibu taifa lililojengwa kwa miaka 60, wanapaswa kuacha mara moja.