` DKT. LUZILA: WATOTO WA GRAMU 600 SASA WANAISHI, NI USHINDI MKUBWA

DKT. LUZILA: WATOTO WA GRAMU 600 SASA WANAISHI, NI USHINDI MKUBWA

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dkt. John Luzila, akizungumza leo Ijumaa Novemba 21,2025 katika maadhimisho ya Siku ya Watoto Wali­ozaliwa Kabla ya Muda (Pre-mature Babies). 

Na Kadama Malunde –  Shinyanga

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dkt. John Luzila, amesema maboresho makubwa ya huduma za watoto wachanga yameiwezesha hospitali hiyo kuokoa maisha ya watoto waliozaliwa na uzito mdogo sana kati ya gramu 600, 800 hadi 900 hali ambayo miaka ya nyuma ilikuwa nadra sana kutokea.

Akizungumza leo Ijumaa Novemba 21,2025 katika maadhimisho ya Siku ya Watoto Wali­ozaliwa Kabla ya Muda (Pre-mature Babies), Dkt. Luzila amesema hatua hiyo ni ushindi mkubwa unaotokana na juhudi za watumishi, wazazi na uwekezaji wa Serikali katika huduma za watoto wachanga.
Dkt. John Luzila

“Zamani mtoto akizaliwa chini ya kilo 1.5 uwezekano wa kuishi ulikuwa mdogo sana. Lakini leo tunawaona watoto wa gramu 600 na 800 wakikua na kuendelea vizuri. Hii ni zawadi kutoka mbinguni na ushindi mkubwa kwa Shinyanga,” amesema Dkt. Luzila.

Ameeleza kuwa, kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), kati ya wanawake 10 wanaojifungua, mmoja hujifungua mtoto aliyezaliwa kabla ya umri, hivyo kuhitaji huduma maalum na ufuatiliaji wa karibu.
"Tangu Januari hadi Oktoba 2025, hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga imehudumia jumla ya watoto 315 waliozaliwa kabla ya wiki 37, hii ni wastani wa watoto 30 kwa mwezi jambo linalothibitisha ukubwa wa changamoto hiyo katika jamii",ameongeza Dkt. Luzila.

Dkt. Luzila ameeleza kuwa Serikali inaendelea kushughulikia changamoto zilizopo, ikiwemo upatikanaji wa vifaa muhimu vya watoto njiti na ukamilishaji wa majengo muhimu ya hospitali.

Akisoma risala, Dkt. Martha Munuo (kutoka Idara ya Watoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga) ameweka bayana mafanikio makubwa ya hospitali hiyo, ikiwemo: Uokoaji wa watoto gramu 600–900 kupitia huduma za NICU, Ushirikiano wa wazazi waliokubali kufanya kangaroo mother care na kufuatilia ukuaji wa watoto pamoja na msaada wa wadau mbalimbali kama Women for Change, Evelyn (Block Manager) Maternity, Blessed Mamaz, Team March, na wahisani wengine wanaoisaidia wodi ya watoto wachanga.
Dkt. Martha Munuo

Hata hivyo amezitaja baadhi ya changamoto zilizopo kuwa ni pamoja na upungufu wa mashine za upumuaji CPAP, flowmeter, infusion pump, na dawa za kukomaza mapafu, udogo wodi na upungufu wa watoa huduma katika NICU.

Aidha ameishukuru Wizara ya Afya na Serikali kwa maboresho makubwa ya miundombinu na huduma katika hospitali hiyo.
Dkt. Gladness Mutajunwa

Kaimu Mkuu wa Idara ya Watoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Gladness Mutajunwa, ameishukuru jamii na wazazi kwa ushirikiano wao kuhakikisha watoto njiti wanakua vizuri.

Naye Daktari Bingwa wa Watoto kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora, Dkt. Linda Paul, ameipongeza Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga kwa kuwa mfano wa kuigwa katika huduma za watoto waliozaliwa kabla ya muda.
Dkt. Linda Paul

“Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga mnafanya kazi kubwa. Huduma mnazozitoa ni za kuigwa nchini,” amesema Dkt. Linda.

Nao Wazazi wametoa shukrani kwa madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Rufaa Shinyanga kwa kuokoa maisha ya watoto wao njiti, wakisema huduma waliyopewa imekuwa ya kiwango cha juu na yenye huruma.
Wamesema bila kujitolea kwa watumishi na ushirikiano wa hospitali, watoto wao wasingefikia hatua ya leo, na wametoa pongezi kwa serikali na wadau wote waliowasaidia katika safari hiyo.

Kauli mbiu mwaka huu ni “Tuwapatie Mwanzo mzuri watoto wanaozaliwa kabla ya muda kwa maisha ya baadae”

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dkt. John Luzila, akizungumza leo Ijumaa Novemba 21,2025 katika maadhimisho ya Siku ya Watoto Wali­ozaliwa Kabla ya Muda (Pre-mature Babies). Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dkt. John Luzila, akizungumza leo Ijumaa Novemba 21,2025 katika maadhimisho ya Siku ya Watoto Wali­ozaliwa Kabla ya Muda (Pre-mature Babies).
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dkt. John Luzila, akizungumza leo Ijumaa Novemba 21,2025 katika maadhimisho ya Siku ya Watoto Wali­ozaliwa Kabla ya Muda (Pre-mature Babies).
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dkt. John Luzila, akizungumza leo Ijumaa Novemba 21,2025 katika maadhimisho ya Siku ya Watoto Wali­ozaliwa Kabla ya Muda (Pre-mature Babies).
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dkt. John Luzila, akizungumza leo Ijumaa Novemba 21,2025 katika maadhimisho ya Siku ya Watoto Wali­ozaliwa Kabla ya Muda (Pre-mature Babies).
Dkt. Martha Munuo (kutoka Idara ya Watoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga akisoma risala wakati wa maadhimisho ya Siku ya Watoto Wali­ozaliwa Kabla ya Muda (Pre-mature Babies).
Wazazi wakiwa kwenye maadhimisho ya Siku ya Watoto Wali­ozaliwa Kabla ya Muda (Pre-mature Babies).
Wazazi wakiwa kwenye maadhimisho ya Siku ya Watoto Wali­ozaliwa Kabla ya Muda (Pre-mature Babies).
Wazazi wakiwa kwenye maadhimisho ya Siku ya Watoto Wali­ozaliwa Kabla ya Muda (Pre-mature Babies).

    Zoezi la kukata kwenye maadhimisho ya Siku ya Watoto Wali­ozaliwa Kabla ya Muda (Pre-mature Babies).
 Zoezi la kukata kwenye maadhimisho ya Siku ya Watoto Wali­ozaliwa Kabla ya Muda (Pre-mature Babies).
 Zawadi zikitolewa kwa wazazi kwenye maadhimisho ya Siku ya Watoto Wali­ozaliwa Kabla ya Muda (Pre-mature Babies).

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464