` MWIGULU NCHEMBA ATEULIWA KUWA WAZIRI MKUU

MWIGULU NCHEMBA ATEULIWA KUWA WAZIRI MKUU

RAIS Samia Suluhu Hassan amemteua Dk. Mwigulu Lameck Nchemba kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,akichukua nafasi iliyokuwa wazi kufuatia mabadiliko ya uongozi serikalini.

Uteuzi huo umetangazwa leo Novemba 13, 2025, ambapo kabla ya nafasi hiyo, Dk. Nchemba alikuwa Waziri wa Fedha.

Dk. Nchemba, ambaye pia ni Mbunge wa Iramba Magharibi mkoani Singida, amewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini ikiwemo Waziri wa Katiba na Sheria, na Waziri wa Mambo ya Ndani.

Mwiguli Nchemba anachukua nafasi ya aliyekuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464