` MOWADITA SHINYANGA YAWAWEZESHA WANAWAKE NA WASICHANA WENYE ULEMAVU KUTAMBUA HAKI ZAO

MOWADITA SHINYANGA YAWAWEZESHA WANAWAKE NA WASICHANA WENYE ULEMAVU KUTAMBUA HAKI ZAO


Na Mwandishi Wetu.

Mradi wa MOWADITA-SHINYANGA umeendelea kuleta mabadiliko chanya katika jamii kupitia utekelezaji wa shughuli za utetezi wa haki na ushawishi kwa wanawake na wasichana wenye ulemavu, sambamba na mafunzo ya ujasiriamali kwa makundi hayo.

Katika mdahalo ulioandaliwa hivi karibuni, washiriki wamepata uelewa mpana kuhusu haki zao za msingi, ikiwa ni pamoja na namna ya kuzitumia vyema fursa mbalimbali zilizopo kwenye jamii ili kujiendeleza kiuchumi na kijamii.

Akizungumza katika mdahalo huo, mmoja wa wawezeshaji alisema hatua hiyo imeongeza mwamko wa wanawake na wasichana wenye ulemavu kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo na kufanya maamuzi yanayohusu maisha yao.

Aidha, washiriki wameelimishwa juu ya mikataba ya kimataifa, sheria, sera na miongozo inayogusa upatikanaji wa haki za watu wenye ulemavu, jambo ambalo limeongeza ujasiri wao wa kudai haki katika maeneo wanayoishi na kufanyiwa kazi kwa masuala yanayowahusu.

Mafunzo ya ujasiriamali yaliyoendeshwa nayo yameelezwa kuongeza uwezo wa wanawake na wasichana hao kuanzisha na kuendeleza miradi midogo ya kiuchumi ili kujipatia kipato na kujitegemea.

Mradi wa MOWADITA-SHINYANGA unaendelea kutekelezwa kwa ushirikiano na wadau mbalimbali wa maendeleo ili kuhakikisha wanawake na wasichana wenye ulemavu wanakuwa sehemu ya maendeleo endelevu katika mkoa wa Shinyanga.

Pamoja na mambo mengine Taasisi ya Mowadita SHINYANGA imeweza kujenga mahusiano baina ya Wanawake na wasichana wenye ulemavu  na kuwawezesha kuunda vikundi vitano vya Wanawake na wasichana wenye ulemavu ambavyo ni  KIKUNDI CHA AMANI, TUPENDANE , UPENDO, COMMUNITY BASED ORGANISATIO ( CBO) NA UKOMBOZI kwa lengo la kuwaweka pamoja na kufanya shughuli za ujasiriamali.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464