Na; Richard Bagolele - Shinyanga
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Wakili Julius Mtatiro amewahimiza wananchi wa Wilayani Shinyanga hususan watumishi wa umma kujenga tabia ya kupima afya mara kwani kutokufanya hivyo kunasababisha magonjwa abayo yangeweza kutibika mapema.
Mhe. Mtatiro ametoa rai hiyo leo wakati wa kikao cha kujadili Utekelezaji wa mktaba wa lishe kwa Wilaya ya Shinyanga kwa kipindi cha Julai hadi Septemba 2025 kilichozikutanisha Halmashauri za Manispaa na Wilaya ya Shinyanga kilichofanyika kwenye ukumbi Mwl. Alexius Kagunze Manispaa ya Shinyanga.
"Ni mhimu zaidi tukajenga tabia ya kufanya vipimo vya afya zetu mara kwa mara sio hadi uugue ndipo uende hospitali kwa ajili ya Matibabu, watumishi na wananchi tujali afya zetu kwani ndiyo kila kitu" amesema Mhe. Wakili Mtatiro.
Mhe. Wakili Mtatiro pia amewashauri akina mama kupima saratani ya shingo ya kizazi angalau mara moja kwa kila miaka miwili ili ugonjwa huo ambao pia umekuwa ni tatizo ambapo amesema magonjwa mengi pia yamekuwa yakisababishwa na msongo wa mawazo pamoja na hali ya maisha kwa ujumla hivyo amesema ni vyema jamii ikabadilika na kujenga tabia ya kufanya vipimo mara kwa mara.
Mhe. Wakili Mtatiro amewataka wataalamu wa afya kutoa elimu ya mara kwa mara kwa watumishi pamoja na wananchi wote ili wachukue tahadhali mapema ya magonjwa hatari katika jamii pamoja na kusisitiza juu ya masuala ya lishe bora katika jamii.
Akiwasilisha taarifa ya Utekekezaji wa lishe kwa Manispaa ya Shinyanga kwa niaba ya mratibu wa Lishe ndugu Misango George amesema katika kipindi cha Julai hadi Septemba 2025, jumla ya watoto 135 walibainika kuwa na utapiamlo mkali ambapo waliandikishwa kwenye matibabu na kati yao watoto 122 wamepona na waliobaki wanaendelea na matibabu katika hospitali na vituonvya afya vya Manispaa ya Shinyanga.
Wakichangia taarifa hiyo wajumbe wameshauri kuendelea na mikakati ya kuhamsisha shughuli za lishe shuleni na kwenye jamii ili kufikia lengo la mkataba wa lishe.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464




