` VYAMA VYA SIASA SHINYANGA VYA TOA TAMKOA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU ,WASISITIZA AMANI

VYAMA VYA SIASA SHINYANGA VYA TOA TAMKOA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU ,WASISITIZA AMANI

Baadhi ya Viongozi wa vyama vya siasa  ambao pia ni wagombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini

 


Mwenyekiti wa Umoja wa vyama vya siasa Mkoa wa Shinyanga Rashid Mohammed akisoma tamko lao kuelekea uchaguzi Mkuu Oktoba 29
  Na Stella Herman,Shinyanga

Ikiwa imebaki siku moja kufika siku ya kupiga kura Oktoba 29,  Umoja wa vyama vya siasa Mkoa wa Shinyanga umewaomba wananchi  kutumia haki yao ya kikatiba kwenda kupiga kura ili kuchagua viongozi wanaowataka.

Hayo yameelezwa leo Oktoba 27,2025 na  Mwenyekiti wa umoja wa vyama vya siasa Mkoa wa Shinyanga Rashid Mohammed, wakati wakitoa tamko la kuwaomba wananchi wenye sifa ya kupiga kura washiriki kikamilifu kupiga kura na kuwaomba wawapuuze watu wanaotoa vitisho kwenye mitandao ya kijamii.

Viongozi hao wamesema vyama vya siasa vimefanya kampeni zake kwa utulivu na amani  hadi sasa wanaelekea siku ya uchaguzi na kuwatoa hofu wananchi kuwa kuna amani ya kutosha na Shinyanga ni salama na amani ipo ya kutosha.

 Katika tamko la viongozi hao wameipongeza serikali ya Mkoa kwa kushirikiana nao katika nyakati zote na kuchukuwa hatua kutatua changamoto zilizokuwa zinajitokeza jambo ambalo limewapa faraja kubwa.

 Mwenyekiti wa umoja wa vyama vya siasa Mkoa wa Shinyanga Rashid Mohammed amesema kuwa jeshi la polisi limekuwa nao sambamba katika kuimarisha ulinzi na usalama hasa wakati wa kampeni zilizokuwa zikifanyika.

Viongozi hao baada ya kutoa tamko lao pia wametumia fursa hiyo kunadi sera za vyama vyao na kueleza mikakati yao,ambapo baadhi ya wagombea ubunge wametumia fursa hiyo kuomba kura kwa wananchi ili wawachague Oktoba 29.

                                        
Baadhi ya Viongozi wa vyama vya siasa  ambao pia ni wagombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini


Baadhi ya Viongozi wa vyama vya siasa  ambao pia ni wagombea ubunge 

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464