Na Marco Maduhu,SHINYANGA
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo jipya la Itwangi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Azza Hillal Hamad, amehitimisha kwa kishindo kampeni za kunadi sera na Ilani ya CCM, huku akiwaomba wananchi wajitokeze kwa wingi Oktoba 29 kupiga kura na kutiki kwa wagombea wote wa CCM.
Kampeni hizo za kufunga zimefanyika leo Oktoba 27, 2025, katika Kata ya Tinde, zikihudhuriwa na maelfu ya wananchi wa Jimbo la Itwangi, huku mgeni rasmi akiwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa.
Azza, akihutubia mamia ya wananchi waliofurika kwenye mkutano huo,amewaomba kumpa kura nyingi za ushindi ili aweze kuwatumikia ipasavyo na kushughulikia changamoto zinazowakabili.
“Wananchi wa Itwangi, kabla hata hamjanipigia kura tayari najua matatizo yenu. Oktoba 29 nipigieni kura nyingi za ushindi ili nipate nafasi ya kuwasemea na kuyatatua,” amesema Azza.
Azza amemndani pia Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisema ni kiongozi jasiri, mnyenyekevu na mwenye kujali maslahi ya wananchi, ambaye ameifanya Tanzania iendelee kukua kimaendeleo.
“Mama Samia ni jasiri na ana mapenzi makubwa kwa wananchi. Ametekeleza miradi mikubwa ya maendeleo, hivyo anapaswa kupewa kura nyingi ili aendelee kuongoza nchi yetu,” amesema Azza.
Ametaja baadhi ya mafanikio yaliyopatikana kupitia Serikali ya Awamu ya Sita chini ya CCM katika Kata ya Itwangi,kuwa ni upatikanaji wa umeme katika vijiji vyote 58, kukamilika kwa maboma ya zahanati, na kuboresha miundombinu ya elimu.
Aidha, ametaja miradi mingine kuwa ni ujenzi wa barabara, madaraja na makavati, sambamba na kuimarika kwa huduma ya maji.
Ameahidi pia kupigania mradi wa maji wa Tinde Package unaolenga vijiji 18, ili kupunguza adha ya maji kwa wananchi wa Itwangi na kwamba kati ya vijini 58 vijiji ambavyo havina huduma ya maji ni 35 tu.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa, amempongeza Azza kuwa ni kiongozi bora wa mfano na moyo wa kujitolea na mwenye kujali maslahi ya wananchi, na kuwataka kumpa kura nyingi ili awe Mbunge wao wa kwanza wa Jimbo la Itwangi.
“Azza ni kiongozi mchapakazi, mpenda maendeleo na mwenye kujali wananchi wake,tumpe kura nyingi ili awe Mbunge wetu na alete maendeleo zaidi,” amesema Mlolwa.
Amemuombea pia kura nyingi za ushindi Rais Dkt Samia Suluhu Hassan,kwamba alipokabidhiwa nchi amefanya mambo makubwa ya kimaendeleo na anapaswa kupewa mitano tena.
Mlolwa amewasihi wananchi wa Itwangi kujitokeza kwa wingi Oktoba 29, siku ya Uchaguzi Mkuu, na kuwachagua wagombea wote wa CCM kuanzia ngazi ya Udiwani, Ubunge hadi Urais.
TAZAMA PICHA👇👇
Mgombea Ubunge Jimbo la Itwangi kupitia CCM Azza Hillal Hamad akinadi sera kwa wananchi wa Itwangi.
Mgombea Ubunge Jimbo la Itwangi kupitia CCM Azza Hillal Hamad akinadi sera kwa wananchi wa Itwangi.
Mgombea Ubunge Jimbo la Itwangi kupitia CCM Azza Hillal Hamad akinadi sera kwa wananchi wa Itwangi.
Mgombea Ubunge Jimbo la Itwangi kupitia CCM Azza Hillal Hamad akinadi sera kwa wananchi wa Itwangi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akizungumza.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akimnadi Mgombea Ubunge Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Edward Ngelela akizungumza.




















































































