` VIONGOZI WA DINI, WAGANGA WA JADI NA WAJASILIAMALI WAAHIDI KUKIPIGIA KURA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM

VIONGOZI WA DINI, WAGANGA WA JADI NA WAJASILIAMALI WAAHIDI KUKIPIGIA KURA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM

 

Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga mjini Fue Mrindoko akiomba kura kwa wananchi wa kata ya Ndembezi 

Suzy Butondo, Shinyangablog

Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Shinyanga mjini imewaomba Viongozi wa dini, waganga wa jadi na wajasiliamali wa kata ya Ndembezi manispaa ya Shinyanga kuwachagua wagombea wa chama cha mapinduzi CCM ili waendelee kufanya maendeleo na kumalizia pale walipoishia.

Licha ya kuwachagua wagombea hao pia imewaomba viongozi wa dini wanapokuwa kwenye maombi wawakumbuke viongozi wanaowachagua ili wasiwe na kiburi cha mamlaka, badala yake wawatumikie wananchi na kushirikiana nao katika kuleta maendeleo.

Hayo yamesemwa leo na mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Fue Mlindoko ambaye aliambatana na katibu Doris Kibabi pamoja na viongozi wa kamati ya utekelezaji ya wilaya ya Shinyanga mjini.

Mrindoko amesema viongozi wa dini, waganga wa jadi,wajasiliamali na wananchi wote wa kata ya Ndembezi ni vizuri wakajitokeza wote siku ya tarehe 29 wakachague viongozi wa chama cha mapinduzi CCM, ambao ni Rais Samia Suluhu Hassan,mbunge wa jimbo la Shinyanga Patrobas Katambi na diwani wa kata hiyo Pendo Sawa ili walete maendeleo katika kata hiyo.

Aidha katibu wa Jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga Doris Kibabi amewaomba waendelee kukiamini chama cha  mapinduzi CCM ili kiendelee kuwatumikia na kuwaletea maendeleo.

"Niwaombe sana viongozi wangu wote tuliokutana hapa tuwachague wagombea wa CCM ili waweze kutuletea maendeleo,lakini pia niwaombe viongozi wa dini mnapokuwa kwenye maombi msisisahau kuwaombea hawa viongozi wetu tunaowachagua ili wasiwe na kiburi cha mamlaka waweze kuwatumikia na kuwaletea maendeleo katika kata yenu hii ya Ndembezi"amesema Kibabi.

Baadhi ya wachungaji waliohudhulia kikao akiwemo Emmanuel Alfred wametoa ushauri kwa mgombea udiwani wa kata hiyo Pendo sawa kwamba wao ni wahanga wa barabara kwa muda mrefu, hivyo wanaomba watakapomchagua diwani  jambo la kwanza awakumbuke barabara, hasa katika mtaa wa Butengwa walikuwa wametelekezwa kabisa.

Pia wameahidi kwamba wagombea wa CCM  watawapakura, lakini wawe wanafika katika maeneo yote na kujua wanahitaji nini, hasa mgombea wa ubunge jimbo la Shinyanga  wanajua ni mchapa kazi na ni msomi anaweza kuteuliwa tena kuwa waziri, lakini kuwa waziri isimzuie kuwatembelea wananchi wake na kujua kero walizonazo,hata akifanya mkutano mmoja inatosha.

"Pia tunakuomba mgombea wetu wa udiwani kile kivuko cha Ndembezi Mazinge tutakapokuchagua ukianzie kukitengeneza, kwani kimekuwa kikihatarisha maisha ya watu kimeshawahi kumpeleka mtu akapoteza maisha,hivyo tunakuomba sana utusaidie kwa hilo"amesema Alfred.

Imamu wa msikiti wa Ndembezi Khamis Nkingo alitoa ushauri kwa mgombea udiwani kwamba atakapochaguliwa awe mtu wa kusikiliza kero mbalimbali za wananchi wake kama alivyokuwa akifanya aliyekuwa diwani wa kata hiyo marehemu Nkulila, na pia wamemshauri awe na kauli nzuri kwa kila mtu kama alivyokuwa Nkulila.

"Na hii awamu tunakuomba ukatutumikie na kutuletea l maendeleo hivyo tukuombe usitutenge ,huko mtaa wa Butengwa na sisi tunahitaji barabara watoto wetu wanapata shida wakati mvua zinaponyesha ili waende shule mpaka wabebwe, ili kuvushwa kwenye maji,pia tupimiwe viwanja vyetu ili viweze kuwa na thamani,"amesisitiza Mlyambele Masanja.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga mjini Fue Mrindoko akiomba kura kwa wananchi wa kata ya Ndembezi 
Katibu wa Jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga mjini Doris Kibabi akiomba kura kwa wananchi wa kata ya Ndembezi

Mgombea udiwani wa kata ya Ndembezi Pendo Sawa akiomba kura 








 Oktoba 29 tunatiki 




























Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464