
Suzy Butondo, Shinyangablog
Katibu wa UWT mkoa wa Shinyanga Habiba Musimu amewataka wananchi wote wa mkoa wa Shinysnga wajitokeze wote kupiga kura tarehe 29 kwa ajili ya kuwachagua wagombea wa chama cha mapinduzi CCM ili waweze kuletamaendeleo na kukuza uchumi wa kila mmoja.
Hayo ameyasema leo wakati akizungumza na Viongozi wa UWT kutoka wilaya ya Shinyanga mjini na vijijini. ambapo amewataka waende kuwahamasisha wanawake na wanaume wote wajitokeze kwenda kupiga kura, kwani siku hiyo kutakuwa na amani hakuna maandamano hata vitisho vya aina yoyote.
"Niwaombe wanawake wenzangu kwa siku chache hizi zilizobaki tusikae tukatulia twendeni wote tukawahamasishe wanawake wenzetu na wanaume ambao ambao mnaishi nao katika maeneo yenu,kila mmoja ahakikishe anahamasisha kwa ajili ya kupiga kura"amesema Habiba.
"Turudi tukawakumbushe wenzetu tarehe 29 wakapige kura kuna wengine wanaweza kuwa na shida furani ya kiafya tukawasaidie jinsi ya kwenda kupiga kura na kila mmoja ana haki ya kupiga kura"ameongeza Habiba.
Aidha katibu amewashukuru viongozi wote kwa kazi waliyoifanya katika uchaguzi wa kura za maoni, hivyo amewataka hata katika uchaguzi mkuu waendelee kufanya kazi ili kuhakikisha wagombea wa CCM wanapata kura nyingi za kishindo.
Katika kikao hicho pia mgombea ubunge viti maalum Christina Mnzava ameshiriki na kuwashukuru wanawake kwa kumwamini tena na kumchagua, ambapo amewaomba waendelee kupambana ili kuhakikisha kura zinapatikana kwa wingi.


















Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464