Na Mwandishi
Wetu.
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Patrobas Katambi, amepewa sifa kemkem akitajwa kuwa kiongozi kijana, shupavu, mnyenyekevu, na mwenye maono makubwa ya kuendeleza maendeleo.
Kutokana
na mafanikio aliyoyapata katika awamu ya sita ya uongozi (2020–2025), Kada wa
CCM, Rahma Kware, amesisitiza kuwa wananchi wa Shinyanga hawana sababu yoyote
ya kubadilisha uongozi bali Katambi anatoshwa na apaswa kupigia kura nyingi za
ushindi siku ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 29.
Kutoka Milioni 800 hadi Bilioni 7: Kuongezeka kwa Makusanyo
Rahma
amemsifia Katambi,kwamba ametekeleza miradi mikubwa ya maendeleo kwa kugusa sekta
zote,na kuleta heshima kubwa katika mji wa Shinyanga.
Rahma
amesema, katika mikutano ya kampeni ya Katambi aliyohudhuria amefarijika
kusikia uimara wa uongozi wake kwa
kuelezea namna alivyoongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, kwamba
awali kilikuwa kikikusanywa kiasi cha fedha wastani wa Shilingi milioni 800
pekee kwa mwaka. Lakini kwa sasa,
makusanyo yameongezeka kwa kasi kubwa na kufikia Shilingi bilioni 7.
Mafanikio Yaliyoainishwa Kisekta:
Ametaja
pia Mafanikio ya Katambi katika jimbo la Shinyanga Mjini yameonekana katika
sekta mbalimbali za kijamii na miundombinu.
Sekta ya Afya
Katika
sekta ya afya, Katambi amesaidia:
- Kufanikisha upatikanaji wa
zaidi ya Shilingi bilioni 7.5 kwa ajili ya kukamilisha jengo la
Hospitali ya Rufaa ya Mwawaza, ambalo sasa limewezeshwa kwa vifaa tiba vya
kisasa, pamoja na upatikanaji wa dawa.
- Kusaidia kupatikana kwa ambulance
nne.
- Kufanikisha ujenzi wa zahanati
nane katika maeneo mbalimbali ya jimbo hilo.
Sekta ya Elimu
Mafanikio
katika elimu ni pamoja na:
- Kuhusishwa na ujenzi wa shule
11 (ambazo ni shule sita za msingi na tano za sekondari).
- Kuanzishwa kwa taasisi za elimu
ya juu zikiwemo Chuo Kikuu cha Ushirika Kizumbi, Chuo cha Madini,
na Chuo cha Serikali za Mitaa.
Miundombinu (Umeme, Barabara, na Maji)
Katika
kuboresha miundombinu, yafuatayo yamefanyika:
- Umeme: Vijiji 55 vimeunganishwa na huduma ya umeme.
- Barabara: Barabara nyingi zilizokuwa hazipitiki sasa zimewekewa madaraja
ya kisasa.
- Maji: Sekta hii imepata mabadiliko makubwa kupitia mtandao
mpya wa maji unaojulikana kama “DP System”, wenye mifumo miwili ya
maji safi na maji taka. Mfumo huu umesababisha gharama ya maji kushuka
hadi Shilingi 1,200 kwa pipa.
Miradi Inayoendelea na Uchumi
Rahma
alisema kuna miradi mingine muhimu inayoendelea ikiwemo ujenzi wa stendi kuu
ya Ibinzamata na barabara ya Mwawaza. Miradi hiyo ameitaja kuongeza kasi ya
ukuaji wa uchumi katika Manispaa ya Shinyanga.
Ahadi za Siku 100 za Rais Samia Madarakani.
Rahma
amenukuu baadhi ya vipaumbele vya Rais
Dkt. Samia Suluhu Hassan kwamba ndani ya siku 100 za mwanzo katika Urais wake,
kwamba ataboresha sekta za elimu, afya, ajira, na kuanzisha mchakato wa Katiba Mpya.
Akizungumzia
ahadi za Rais Samia, Rahma Kware alitaja mipango miwili mikuu:
1.
Afya kwa Wote: Rais ameahidi kuzindua Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
kwa Wote, ambao utagharamia matibabu kwa makundi maalum kama vile wazee,
watoto, mama wajawazito, na watu wenye ulemavu.
2.
Uwezeshaji
Kiuchumi: Serikali imetenga Shilingi
bilioni 200 kwa ajili ya kuwawezesha wafanyabiashara wadogo, bodaboda, mama
lishe, na wajasiriamali wadogo kunufaika na huduma rasmi.
Wito kwa Wananchi wa Shinyanga
Rahma
alihitimisha kwa maneno haya: "Waswahili wanasema mnyonge mnyongeni lakini
haki yake mpeni. Katambi anatutosha"huku akitoa wito kwa Wanashinyanga
kwenda kumshukuru Katambi kwa kumpa kura
nyingi za kishindo ili arudi kuwatumikia tena kwa awamu nyingine, pamoja
na ushindi mnono kwa Rais.Dkt Samia Suluhu Hassan.
