` TCRS YAADHIMISHA KUMBUKIZI YA KIFO CHA MWL NYERERE KWA BONANZA LA MICHEZO SHAGIHILU,YAHAMASISHA UTUNZAJI MAZINGIRA

TCRS YAADHIMISHA KUMBUKIZI YA KIFO CHA MWL NYERERE KWA BONANZA LA MICHEZO SHAGIHILU,YAHAMASISHA UTUNZAJI MAZINGIRA

 Afisa Mradi wa TCRS, Mwanamina Mavura akizungumza kwenye bonanza la MICHEZO lenye lengo la kuwajengea uwezo wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi lililofanyika katika uwanja wa Kijiji Cha Shagihilu Kata ya Shagihilu Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Oktoba 14,2025

Na Sumai Salum – Kishapu

Shirika la Tanzania Christian Refugee Service (TCRS) limeadhimisha kumbukizi ya miaka 29 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kuandaa bonanza la michezo lililofanyika katika Kijiji cha Shagihilu, Kata ya Shagihilu, Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga.

Bonanza hilo limefanyika Oktoba 14,2025 kwenye uwanja wa Kijiji huku likiambatana na michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, ngoma za asili, nyimbo, ngonjera, na mchezo wa kukimbiza kuku na maonesho ya wajasiliamali. Katika mashindano ya mpira wa miguu, Shagihilu FC imeibuka mshindi wa kwanza, ikifuatiwa na Mangu FC huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Mwatuju FC.


Akizungumza katika hafla hiyo, Afisa Mradi wa TCRS, Mwanamina Mavura, amesema lengo la bonanza hilo ni kuwaleta wananchi pamoja na kuwajengea uwezo wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi. Ametoa elimu kuhusu utunzaji wa mazingira, upandaji miti, matumizi ya nishati safi ya kupikia, lishe bora, ufugaji wa kisasa, kilimo bora na ujasiriamali kama njia endelevu za kujikwamua kiuchumi.

Mwanamina ametumia fursa hiyo kuipongeza serikali ya Wilaya kwa ushirikiano mkubwa tangu kuanzishwa kwa mradi huo wa "Kujengea Jamii Uwezo Kukabili Mabadiliko Tabianchi"mwaka 2022, akibainisha kuwa unatarajiwa kukamilika Disemba 2025. Amesema ushirikiano huo umekuwa chachu ya mafanikio makubwa katika utekelezaji wa shughuli za utunzaji wa mazingira na kuimarisha uchumi wa kaya.

"Kipekee kabisa Kwa niaba ya TCRS nipende kutoa pongezi za dhati kwenu Wananchi wote wa Kata ya Shagihilu Kwa muitikio mkubwa mliouonesha Leo hata kukubali kuacha shughuli zenu na kuja kwenye bonanza Hilo na zaidi sana kukubaliana na elimu inayotolewa kuhusu utunzaji wa mazingira na hata sasa tunaona jamii ikiwa na mabadiliko Kwa kiwango kikubwa pia tuendelee kushirikiana kupinga ukatili na ukataji wa miti hovyo" amesisitiza Meneja mradiMtendaji wa Kata ya Shagihilu Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga na mgeni rasmi Simon Lue akizungumza kwenye bonanza la michezo lililoandaliwa na Shirika la TCRS lenye lengo la kuwajengea uwezo wananchi wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi lililofanyika katika uwanja wa Kijiji Cha Shagihilu Oktoba 14,2025

Kwa upande wake, Mtendaji wa Kata ya Shagihilu,Simeon Lue, ambaye alikuwa mgeni rasmi, ameipongeza TCRS kwa ubunifu wa kutumia michezo kuimarisha umoja wa wananchi na kukuza elimu ya mazingira. Amesisitiza kuwa serikali ya Wilaya ya Kishapu itaendelea kushirikiana na wadau wote wanaotekeleza miradi inayolenga kuboresha maisha ya wananchi vijijini.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Shagihilu Kata ya Shagihilu Wilayani Kishapu Mkaoni Shinyanga Nickson limbe akizungumza kwenye bonanza la michezo lililoandaliwa na Shirika la TCRS lenye lengo la kuwajengea uwezo wananchi wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi lililofanyika katika uwanja wa Kijiji Cha Shagihilu Oktoba 14,2025

Mwananchi wa Shagihilu, Consolatha Victor, amesema bonanza hilo limekuwa na manufaa makubwa kwa wanawake kwa kuwaelimisha kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia na namna ya kukabiliana na changamoto za tabianchi.

Mwanachi mwingine Gaudencia Manje amesema mpango huo umeendelea kuwa chachu ya mabadiliko kwa jamii, kwani unawawezesha wananchi kujitegemea, kulinda afya zao, na kuendesha shughuli zao za kiuchumi kwa tija.Mwananchi wa Shagihilu Kata ya Shagihilu Wilaynai Kishapu Mkoani Shinyanga Consolatha Victor

Mchezaji wa timu ya Mwatuju FC, Matius Masanja amesema wamevutiwa na bonanza hilo kwa kuwa limewaunganisha vijana na kuwajengea moyo wa mshikamano, huku wakikumbuka falsafa ya Mwalimu Nyerere ya umoja na upendo kwa maendeleo ya Taifa.

Mradi huo wa “Kujengea Jamii Uwezo wa Kukabili Mabadiliko ya Tabianchi” unatekelezwa kwa ufadhili wa Shirika la Felm kupitia Wizara ya Mambo ya Nje ya Finland, na unatekelezwa katika kata nne za Wilaya ya Kishapu ambazo ni Shagihilu, Ndoleleji, Masanga na Mwakipoya.Mwananchi wa Shagihilu Kata ya Shagihilu Wilaynai Kishapu Mkoani Shinyanga Consolatha VictorMchezaji wa timu ya Mangu FC iliyoko Kata ya Shagihilu Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Matius Masanja

Kwa mujibu wa taarifa ya mradi huo, malengo yake makuu ni pamoja na:

▪️Kuimarisha usalama wa chakula kwa kutumia mbinu bora za kilimo na ufugaji.

▪️Kuongeza fursa za kiuchumi kupitia usimamizi wa shughuli za ujasiriamali na upatikanaji wa huduma sahihi za masoko.

▪️Kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi kwa kukuza uwezo wa jamii katika utunzaji wa mazingira na upandaji miti.

▪️Kujenga jamii inayobadilika kitabia ili kupata maendeleo endelevu kupitia ushiriki wa vijana na wanawake katika shughuli za uhifadhi wa mazingira.

Shagihilu Fc imeibuka kidedea kwa ushindi wa goli moja kwa sifuri dhidi ya Mangu Fc goli hilo lilifungwa na kiungo namba saba Mkumbo Michael kipindi cha pili dakika ya 64 wakiondoka na kombe,jezi,mipira 2 na fedha taslimu,huku mshindi wa pili Mangu Fc akiondoka na mpira 1,jezi na fedha taslimu alikadhalika msindi wa tatu Mwatuju Fc.Kiungo namba saba timu ya Shagihilu Fc Mkumbo Michael aliyewapa ushindi na kuibuka kidedea bonanza la TCRS na utunzaji mazingira Oktoba 14,2025

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464