MNDUMBWE SEKONDARI YASHIKA NAFASI YA KWANZA TANDAHIMBA
Na. Beatus Bihigi - Mtwara
Shule ya sekondari Mndumbwe ni miongoni mwashule mpya zinazo fanya vizuri sana kitaaluma, ambapo ilianzishwa rasmi 2023 chini ya Mkuu wa shule Ntarisa Kisyeri Ntarisa.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida Wanafunzi wa kidato cha pili shuleni hapo wameibuka washindi wa kwanza katika mtihani wa taifa wa kujipima (Pre national/Mock), huku wakiziburuza shule kongwe na zenye majina makubwa katika wilaya hiyo Tandahimba.
Aidha Mndumbwe sekondari imeongoza kwa kushika nafasi ya kwanza (1) kiwilaya kati ya shule 31 na kushika nafasi ya 18 kimkoa.
Mkuu wa shule hiyo Mwl.Ntarisa K. Ntarisa amewapongeza walimu na Wanafunzi wote kwa matokeo mazuri sana kuwahi kutokea, ambapo amefanya hafla fupi kwa kuchinja mbuzi dume na kuchoma mishikaki iliyotanguliwa na supu kwa walimu wote.
Aidha Wanafunzi wote amewapongeza kwa kuwanunulia gunia la mchele kilogram 100 na kutoa fedha kwa kila mwanafunzi wa kidato cha pili aliyepata daraja la kwanza (Division One).
"Nimeleta walimu wa masomo ambayo hayana walimu mfano Business Studies kwa kidato cha kwanza na Elimu ya Dini ya Kiislamu -EDK kwa madarasa yote, sasa nawaomba mjitume kusoma ili mfanye vizuri zaidi na mimi nitaendelea kutoa zawadi kadri iwezekanavyo", alisema Ntarisa ambaye ndiye Mkuu wa shule Mndumbwe sekondari Tandahimba Mkoani Mtwara.
Sambamba na hilo hafla hiyo ilijumuisha Afisa watendaji kata na Kijiji cha Mndumbwe Bw. Nicolas Matonya na Yohana Mapunda ambao walipongeza uongozi wa shule, Mkuu wa shule na walimu wote kwa jitihada zao hususan ofisi ya taaluma inayosimamiwa na Mwl. Mathayo M. Kwaslema akishirikiana na Mwl.Beatus Stephen Bihigi.
