` SALUM KITUMBO:NIMEKUJA KUWAPELEKA WANANCHI WA SHINYANGA MJINI KWENYE NCHI YA ASALI NA MAZIWA

SALUM KITUMBO:NIMEKUJA KUWAPELEKA WANANCHI WA SHINYANGA MJINI KWENYE NCHI YA ASALI NA MAZIWA

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MGOMBEA udiwani Kata ya Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Salum Kitumbo,amenadi sera na ilani ya CCM kwa wananchi wa Kata hiyo,huku akiwahidi wakimpatia ridhaa ya kuwa Diwani wao atawapeleka kwenye nchi ya Asali na Maziwa sababu ya kutekeleza miradi mingi ya maendeleo na kutatua changamoto zao zote.
Amebainisha hayo leo Oktoba 3,2025 kwenye Mkutano wake wa Kampeni wa kunadi sera kwa wananchi,ili wamchague Oktoba 29 siku ya Uchaguzi Mkuu awe diwani wao,pamoja na kumuomba kura nyingi za Ushindi Rais Dk.Samia Suluhu Hassan na Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi.

Amesema yeye amekuja kama Mussa, katika Kata hiyo ya Shinyanga Mjini, kwa kuwatoa wananchi kwenye nchi ya Misri kuwapeleka Kaanani, nchi ya Asali na Maziwa, na kwamba akipata ridhaa hiyo ya kuwa diwani wazee wote wa Kata hiyo watapata bima za afya bure.

Ametaja vipaumbele vingine kuwa ni kuhakikisha vijana, wanawake na watu wenye ulemavu ambao wamejiunga kwenye vikundi wanapata mikopo ya halmashauri asilimia 10 ili wapate kujikwamua kiuchumi.
“Mimi mkinipatia ridhaa ya kuwa diwani wenu siku ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 29 nitawapeleka kwenye nchi ya Asali na Maziwa naombe msifanye makosa,mpigie pia kura nyingi za Ushindi Rais wetu Dk.Samia Suluhu Hassani na Patrobas Katambi,ili tufanye kazi kwa ushirikiano na kuwaletea maendeleo,”amesema Kitumbo.

Aidha,amewahidi vijana watakuwa wakinufaika na fursa ambazo hujitokeza katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa kupewa kipaumbele kwanza,ili wapate kunufaika nazo na kujikwamua kiuchumi.
Pia,ameahidi kuinua michezo hapa Shinyanga ikiwamo kuboresha viwanja vya michezo, pamoja na miundombinu ya shule kwa kujenga jiko la kisasa shule ya Msingi Mwenge,kuweka umeme kwenye baadhi ya Majengo ambayo hayana huduma hiyo,na kuboresha pia mitaro ya shule ya Sekondari Buluba.

Nao viongozi mbalimbali wa Chama waliohudhuria mkutano huo wa Kampeni,wamemueleza Kitumbo kuwa ni kiongozi mzuri mwenye maono,pamoja na mpigania maslahi ya wananchi,kwamba Kata ya Shinyanga wamepata diwani ambaye ni jembe.

TAZAMA PICHA👇👇
Mgombea Udiwani Kata ya Shinyanga Mjini kupitia CCM Salum Kitumbo akinadi sera kwa wananchi kwenye Mkutano wa Kampeni.

Meneja Kampeni wa Mgombea Udiwani Kata ya Shinyanga Mjini kupitia CCM, Abubakari Mukadamu akimdani Mgombea wake kwa wananchi.
Meneja Kampeni wa Mgombea Udiwani Kata ya Shinyanga Mjini kupitia CCM, Abubakari Mukadamu (kulia)akimdani Mgombea wake kwa wananchi Salum Kitumbo(kushoto).
Mwenezi wa CCM Kata ya Shinyanga Mjini Sitta Salehe akizungumza kwenye mkutano huo wa Kampeni.
Mwenezi wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Said Bwanga akizungumza kwenye mkutano huo wa Kampeni.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464