` AZZA AWASEMEA WANANCHI WA ITWANGI KWA RAIS.DKT SAMIA SULUHU HASSAN MKUTANO WA KAMPENI,NEEMA YAJA MRADI WA UMWAGILIAJI NYIDA

AZZA AWASEMEA WANANCHI WA ITWANGI KWA RAIS.DKT SAMIA SULUHU HASSAN MKUTANO WA KAMPENI,NEEMA YAJA MRADI WA UMWAGILIAJI NYIDA

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MGOMBE Ubunge wa Jimbo jipya ya Itwangi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Azza Hillal Hamad,amewasilisha maombi ya wananchi wa jimbo hilo kwa mGombea Urais wa CCM,Rais Dkt Samia Suluhu Hassan,ombi la kukamilishwa kwa mradi wa maji Tinde Package ambao umekuwa ukisuasua wa vijiji 18, na ukamilishaji mradi wa umwagiliaji Nyida na kuongezwa kwa hekali 390.

Azza,ametoa maombi hayo leo Oktoba 11,2025 kwenye mkutano wa kampeni wa Rais Dkt,Samia uliofanyika katika Uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga,wa kunadi sera na ilani ya CCM kwa wananchi.
Amesema, ndani ya miaka minne ya Utawala wa Rais Dkt Samia katika Jimbo hilo la Itwangi,miradi mingi ya maedeleo imetekelezwa ikiwamo ya kimkakati, ujenzi wa miundombinu ya Barabara na Zahanati.

“Mheshimiwa Mgombea wa Urais,pamoja na mambo makubwa ambayo yamefanyika Itwangi naleta maombi,tuna mradi mkubwa wa maji ambao umekuwa ukisuasua unaitwa Tinde Package, utakaochukua vijiji 18,na shauku kubwa ya wananchi wa Itwangi katika vijiji hivi ni kupata majisafi na salama,tuna omba Mheshimiwa waukamilishe na kuondoa changamoto ya ukosefu wa maji,”amesema Azza.
Amesema katika Vijiji 58 vya Itwangi,Vijiji 14 ndiyo vinahuduma ya majisafi na salama kutoka mradi wa maji ya Ziwa Victoria, na Vijiji 9 wana Maji ya Visima virefu, na Vijiji 35 havina maji kabisa, na kwamba kukamilika kwa mradi huo wa maji Tinde Package utapunguza adha ya maji kwa wananchi.

Aidha,ameomba ombi jingine la ukamilishwaji wa mradi wa maji wa umwagiliaji wa Nyida ambao una Hekali 840 na kwamba Hekal 450 ndizo zimefanyiwa kazi, na kuomba hekali 390 zilizobaki nazo ziingizwe kwenye utekelezaji wa mradi huo.
Ameongeza ombi jingine kupitia mradi wa SGR,anaomba ujenzi wa Barabara ya lami kutoka Njiapanda ya Didia kwenda Didia Kilomita 5 iwekewe lami,pamoja na ukamlishwaji wa Maboma ya zahanati na vyumba vya madarasa.

Naye Waziri wa Kilimo Hussein Bashe akizungumza kwenye Mkutano huo wa Kampeni,amesema mwaka 2019-2020, kwamba Azza kipindi hicho alipokuwa Mbunge wa Vitimaalum,alimpeleka kwenye mradi huo wa umwagiliaji Nyida, na kwamba mwaka 2024 zilitolewa fedha, na mradi huo hadi sasa umefikia asilimia 87 ya utekelezwaji wake, na kwamba ombi la kuongezwa Hekal zingine 390 tayari zimeshatangazwa na utekelezaji utaanza hivi karibuni.

Mgombea Urais Dkt Samia Suluhu Hassan,amesema maombi yote ambayo yameombwa ameyachukua na watakwenda kuyafanyia kazi na mengine tayari Mawaziri wameshatolea majibu.

Pia,amewaomba wananchi wa Shinyanga kwamba siku ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 29 wajitokeze kwa wingi kupiga kura pamoja na kumchangua yeye pamoja na Wabunge na Madiwani wote wa CCM ili waendelee kuwaletea maendeleo.

TAZAMA PICHA👇👇
Mgombea Urais kupitia CCM Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. akizungumza kwenye mkutano wa kampeni.
Mgombea Ubunge wa Jimbo Jipya ya Itwangi kupitia CCM Azza Hillal Hamad akizungumza kwenye mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais,Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464