` KATAMBI AMWAGA SERA ZA CCM KWA WANANCHI CHAMAGUHA AELEZEA MIRADI YA MAENDELEO ALIYOITEKELEZA

KATAMBI AMWAGA SERA ZA CCM KWA WANANCHI CHAMAGUHA AELEZEA MIRADI YA MAENDELEO ALIYOITEKELEZA

KATAMBI AMWAGA SERA ZA CCM CHAMAGUHA AELEZEA MIRADI YA MAENDELEO ALIYOITEKELEZA

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Patrobas Katambi,ameendelea na mikutano yake ya Kampeni ya kunadi sera na ilani ya CCM kwa wananchi, ili wawa chague wagombea wote wanaotokana na CCM kwenye Uchaguzi Mkuu Oktoba 29 mwaka huu.
Leo Oktoba 1,2025 Katambi amefanya mkutano wa Kampeni katika Kata ya Chamaguha, mbali na kumnadi Mgombea Udiwani wa Kata hiyo Elias Masumbuko, pia ameelezea miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo ameitekeleza kwa wananchi.

Amesema Kata hiyo ya Chamaguha kabla ya kuwa Mbunge mwaka 2020, ilikuwa ikikabiliwa na Changamoto mbalimbali ikiwamo Ubovu wa miundombinu ya Barabara na Madaraja, lakini kero hizo alizifanyika kazi na sasa wanampango wa kuweka Lami na kufungua barabara za mitaa.
Amesema pia katika Shule ya Sekondari Chamaguha wamejenga vyumba vya Madarasa kutoa Vifaa vya TEHAMA na Vitabu vya Sayansi.

“Hapa Chamaguha tumefanya kazi kubwa sana ya maendeleo,tumejenga daraja la milioni 428, ambapo daraja la awali lilibomoka tukajenga jipya, na kuunganisha na Iwelyangula Kata ya Kitangili,”amesema Katambi.
Amesema pia wamejenga Soko jipya la Mbao, ambalo linachangiza uchumi wa wananchi wa Chamaguha, wamejenga na Jengo la Utawala la Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga litakalosaidia kuboresha huduma kwa wananchi.

Katambi,ametaja mikakati mingine ni kujenga pia Ofisi ya Mtendaji wa Kata na wanampango wa kuangalia hifadhi ya ardhi ili kuweka viwanda.
Amesema pia Zahanati ya Kata hiyo wataipandisha ile kiwe Kituo cha Afya kutoka na kuwapo na Idadi kubwa ya wananchi,kwa ajili ya kuboresha huduma za matibabu kwa wananchi.

“CCM ikiahidi inatekeleza miradi yote ambayo tumeitekeleza hapa Chamaguha na Jimbo zima la Shinyanga inaonekana kwa macho na siyo simulizi tu,hivyo nawaomba wananchi Oktoba 29 kura nyingi kwa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan, na mimi ili niendelee kuwa Mbunge wenu pamoja na Madiwani wote wa CCM,”Amesema Katambi.

Mgombea Udiwani wa CCM Kata ya Chamaguha Elias Masumbuko, ambaye alikuwa Meya wa Manispaa ya Shinyanga, amemwagia Sifa Katambi kwamba ni kiongozi ambaye anajali maslahi ya wananchi na amechangiza maendeleo makubwa katika Manispaa hiyo.

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Anold Makombe,amesema Jimbo la Shinyanga Mjini limekuwa na maendeleo makubwa na hivyo kuwasihi wananchi Oktoba 29 wakatiki kwa Rais Samia,Mgombea Ubunge Katambi na Madiwani wote wa CCM ili waendelee kuwaletea maendeleo.

Katibu wa siasa,uenezi na mafunzo CCM Mkoa wa Shinyanga Richard Masele,akizungumza kwenye kampeni hizo, amesema Katambi pamoja na Rais Samia wamefanya kazi kubwa ya kuwaletea maendeleo wananchi, hivyo Oktoba 29 ni kuwapatia kura nyingi za ushindi pamoja na madiwani wote wa CCM.

TAZAMA PICHA👇👇

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi akinadi sera kwa wananchi wa Chamaguha.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (CCM)Patrobas Katambi (kushoto)akimnadi kwa wananchi Mgombea Udiwani Kata ya Chamaguha Elias Masumbuko.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Anold Makombe akizungumza kwenye Mkutano huo wa Kampeni.
Katibu wa siasa,uenezi na mafunzo CCM Mkoa wa Shinyanga Richard Masele,akizungumza kwenye mkutano huo wa kampeni.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464