` MGOMBEA URAIS WA SAU AMWAGA SERA KWA WANANCHI WA SHINYANGA WAMCHAGUE OKTOBA 29

MGOMBEA URAIS WA SAU AMWAGA SERA KWA WANANCHI WA SHINYANGA WAMCHAGUE OKTOBA 29

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MGOMBEA Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Sauti ya Umma (SAU)Majalio Kyara,amenadi sera na ilani ya chama hicho kwa wananchi wa Shinyanga,ili wamchague awe rais na kuwaletea ukombozi wa maendeleo.
Amenadi sera hizo leo Oktoba 1,2025 kwenye Mkutano wa Kampeni uliofanyika katika Stendi ya Mabasi ya wilaya ya Shinyanga.

Amesema, endapo wananchi wakampatia ridhaa ya kuwa Rais wa Tanzania Oktoba 29 mwaka huu kwenye Uchaguzi Mkuu,kwamba atawaletea maendeleo ya kweli pamoja na kuzalisha ajira milioni 10 kwa mujibu wa ilani ya chama hicho.
“Nawaomba wananchi wa Shinyanga siku ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 29 msifanye makosa, bali mnipigie kura nyingi za ushindi,na Wagombea wote wa Ubunge SAU na Madiwani,ili tuwaletee ukombozi wa maendeleo,”amesema Kyara.

Amesema, pamoja na ahadi nyingine ataongeza idadi ya machinjio mikoani na vijijini, ili kuongeza thamani ya mifugo na hakuna tena kusafirisha mifugo kwenda Jijini Dar es salaam.
Ametaja ahadi nyingine,kuwa ni kushusha bei ya mafuta, ili usafirishaji uwe rahisi, pamoja na Wakulima kusafirisha mazao yao kwa gharama nafuu.

Naye Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama hicho Rehema Bulilo, amesema akipata ridhaa ya kuwa Mbunge wa Jimbo hilo,kwamba atahakikisha anapambana kuondoa mikopo kausha damu,kupunguza gharama kubwa za matibabu Hospitalini na kutoa Pembe Jeo bure kwa Wakulima.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464