` KAMPENI YA TUWAAMBIE KABLA HAWAJAHARIBIWA AWAMU YA PILI IMEZINDULIWA RASMI,WANAOKATISHA NDOTO ZA WANAFUNZI WAONYWA

KAMPENI YA TUWAAMBIE KABLA HAWAJAHARIBIWA AWAMU YA PILI IMEZINDULIWA RASMI,WANAOKATISHA NDOTO ZA WANAFUNZI WAONYWA

                                 

   Matembezi ya uzinduzi wa Kampeni ya Tuwaambie kabla hawajaharibiwa awamu ya pili 

 
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi akiwa na viongozi wengine kwenye picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa kampeni ya "Tuwaambie kabla hawajaharibiwa  awamu ya pili.

 Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga leo Septemba 29,2025 limezindua rasmi Kimkoa Kampeni ya Tuwaam bie mapema kabla hawajaharibiwa katika Wilaya  ya  kipolisi Ushetu ,kwa lengo la kuwalinda watoto kutimiza ndoto zao.

Akizindua Kampeni hiyo Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi amesema huo ni mpango mahususi unaosimamiwa na kitengo cha Dawati la jinsia na watoto ili kuongeza uelewa kwa Jamii.

Amesema kampeni hiyo inalenga kujenga Jamii yenye misingi ya heshima,usalama na ulinzi wa mtoto kwa kuwawezesha kutimiza ndoto zao na siyo kujiunga na makundia ambayo hayana tija na yanaweza kuwaharibia mwelekeo.


  
                                         
Amesema lengo la kampeni hiyo kuyawezesha makundi hayo yanakuwa salama dhidi ya vitendo vya ukatili  pia kuwajenga kuwa wazalendo kwa kutoa elimu dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Amesema wamelenga kuondoa au kupunguza vitendo vya ukatili wa kijinsia na kuielimisha jammii kutambua kuwa vitendo vya udhalilishaji ni kosa la jinai na kuripoti ili kuchukuwa hatua za kisheria.



















 

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464